Habari za Michezo
Habari za michezo

HUYU HAPA MTZ ALIYEPATA SHAVU LA KUKIPIGA NA MESSI MAREKANI…

admin February 11, 2024 8:56 pm

FOWADI mwenye asili ya Zanzibar, Amahl Pellegrino amekamilisha usajili kwa kujiunga na San Jose Earthquakes ya Marekani akitokea Bodø/Glimt ya Norway kwa uhamisho wa zaidi ya sh. 700milioni akimfuata mwanasoka bora wa dunia, Lionel Messi.

Pellegrino ambaye ameondoka Ulaya akiwa miongoni mwa washambuliaji hatari, ameshindwa kuficha kwa kusema ubora wa Ligi ya Marekani kwa sasa ni miongoni mwa sababu ambayo imemsukuma kufanya maamuzi hayo.

“Nimecheza mpira Ulaya kwa miaka mingi, nadhani ni wakati sahihi wa kukabiliana na changamoto mpya sehemu nyingine. Ligi ya Marekani ni miongoni mwa ligi nzuri na zenye mvuto,” alisema.

Uhamisho wa Pellegrino kutoka Bodø/Glimt hadi San Jose Earthquakes umepokelewa vizuri na mashabiki pamoja na wachambuzi wa klabu hiyo.

Taarifa ya utambulisho wake ilieleza,”Akiwa na umri wa miaka 33, Pellegrino analeta uzoefu mkubwa na rekodi ya kuvutia ya kufunga mabao. Usajili wake unalenga kuimarisha safu yetu ya ushambuliaji, tunataka kushindana kwa kiwango cha juu ndani na kimataifa.”

San Jose Earthquakes ilionekana kuwa na pengo kwenye safu yake ya ushambuliaji kufuatia kuondoka kwa Cade Cowell kwenda Chivas, hivyo kutua kwa Mzanzibar huyo kunatazamwa kama suluhu.

Wakati akicheza soka la kulipwa Norway, Pellegrino alishinda tuzo mbili za Kiatu cha Dhahabu na akatawazwa Mchezaji Bora wa Mwaka mnamo 2023.

Mwanaspoti. Kata kiu ya michezo na burud

ODDS ZA FAINAL YA AFCON KWA LEO HIZI HAPA…UKIWEKA HIZI USHINDI NI UHAKIKA… UWANJA WA  YANGA SASA MAMBO NI BAMBAM…GSM KUMWAGA MPUNGA WA MAANA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply