Habari za Simba SC
Habari za michezo

INONGA NDANI YA NYUMBA SIMBA IKIVAANA NA SINGIDA LEO….

admin March 12, 2024 1:48 pm

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amesema wanamshukuru Mungu kuona nyota wao wote waliokuwa majeruhi wanarejea kikosini.

Ahmed amesema, nyota wao Willy Onana ambaye alikuwa nje kwa muda kidogo, alirejea na wiki iliyopita alifanya balaa kwa kuwapa goli la ushindi dhidi ya Coastal Union pale Mkwakwani Stadium jijini Tanga lakini pia Henock Inonga naye amerejea.

“Inonga amerejea baada ya kupata majeraha kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons, ameanza mazoezi na wenzake na huwenda akawa sehemu ya mchezo wetu dhidi ya Singida FG,” alisema Ahmed.

Simba anashuka dimbani leo katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar kukipiga na Singida FG ukiwa ni mchezo wao wa 18. Mpaka sasa, Simba ana alama 39 huku mpinzani wao wa jadi Yanga akiwa amecheza michezo 18 tayari akiwa na alama 49.

Endapo Simba akishinda leo na kuchukua alama tatu, atakuwa amepigwa gepu la alama 7 na Yanga.

KAMWE:- KWA HIZI 5G….WALIOSAJILI ‘JOBLESS NA FREDY VUNJA BEI’ WAJIANDAE NA KULA 10G.. KUHUSU GOLI LAKE LA JANA ….MAXI AVUNJA UKIMYA…AFUNGUA UGUMU ANAOPITIA YANGA….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply