Kawempe Muslim Ladies Simba Queens
Michezo Bongo

Kawempe Yafikia Rekodi ya Simba Queens Ligi ya Mabingwa Afrika

Vardo November 10, 2026 9:17 am

REKODI ya miaka minne iliyowekwa na Simba Queens katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Wanawake (CAF WCL) hatimaye imefikiwa! Klabu ya Kawempe Muslim Ladies ya Uganda imekuwa timu ya pili pekee kutoka Ukanda wa CECAFA kutinga hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo makubwa barani Afrika.

Kawempe imekata tiketi hiyo baada ya kuichapa USFA Bamako ya Mali mabao 3-0 katika mchezo wao wa mwisho wa Kundi B uliopigwa nchini Misri. Katika mchezo huo, Jovia Nakagolo alifungua ukurasa wa mabao dakika ya 40 kabla ya Agnes Nabukenya kupiga mabao mawili kipindi cha pili na kuhitimisha ushindi huo mnono.

Simba Queens Walivyoweka Alama 2022

Mwaka 2022, Simba Queens iliandika historia nchini Morocco kwa kuwa timu ya kwanza kutoka Ukanda wa CECAFA kufika nusu fainali.

Baada ya kupoteza mchezo wa kwanza 1-0 dhidi ya AS FAR Rabat, Wanalimbwende hao wa Msimbazi walirejea kwa kasi na kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Determine Girls (Liberia) na kisha kuichapa Green Buffaloes ya Zambia 2-0 kuifuzu nusu fainali, ambapo safari yao iliishia kwa kufungwa 1-0 na Mamelodi Sundowns.

Tofauti ya Kawempe na Timu Nyingine za CECAFA

Tangu mafanikio hayo ya Simba Queens mwaka 2022, timu nyingine zote za CECAFA zilizoshiriki zilipambana lakini ziliishia hatua ya makundi:

  • Vihiga Queens (Kenya) – 2021

  • JKT Queens (Tanzania) – 2023 & 2025

  • Commercial Bank of Ethiopia (CBE) – 2024

Kawempe Muslim Ladies, inayoshiriki fainali hizi kwa mara ya kwanza, imeanza kwa kishindo baada ya kuichapa AS FAR Rabat mabao 3-2, kabla ya kufungwa 2-1 na AMPEM Darkoa ya Ghana na kisha kumaliza kazi dhidi ya USFA Bamako.

Ushindi huo umewafanya kufikisha pointi sita, kushika nafasi ya pili kwenye Kundi B, na kuungana rasmi na Simba Queens kwenye vitabu vya historia vya soka la wanawake ukanda wa CECAFA.

Zimbwe JR Afunguka Ujio wa Fadlu Davids Yanga SC: “Ligi Kuu na CAFCL Tutawashtua!