Simba SC Kutaka Pointi 45 Ligi Kuu: Ahmed Ally Afichua Mipango Mizito!
Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, ameweka wazi kuwa klabu hiyo haijaridhika na mafanikio ya kukusanya pointi 30 katika michezo 10 ya kwanza ya Ligi Kuu ya Tanzania (NBC Premier League), badala yake lengo lao kuu ni kushinda mechi zote 15 na kufikisha pointi 45 mzunguko wa kwanza.
Simba SC imeanza msimu huu kwa kasi ya hatari ikiwa imeshinda michezo yote 10 iliyocheza. Akizungumzia uimara wa kikosi hicho, Ahmed Ally ameeleza kuwa timu hiyo imeonyesha kiwango cha juu na uwezo mkubwa wa kupambana dhidi ya wapinzani wao wakuu wa ubingwa.
βUkiangalia mazingira ya kuzifunga timu zote ambazo tunawania nazo ubingwa, lakini pia kufanya comeback mbili katika michezo 10, maana yake ni kwamba Simba ya safari hii iko tofauti sana na ina kiu kubwa ya mafanikio,β amesema Ahmed Ally.
Lengo ni Pointi 45 Mzunguko wa Kwanza Ahmed amesisitiza kuwa pamoja na kufikisha pointi 30, bado hawana sababu ya kuridhika kwani safari ya kusaka ubingwa ni ndefu. Mpango mkuu wa Wekundu wa Msimbazi ni kumaliza mzunguko wa kwanza bila kupoteza wala kutoka sare mchezo wowote ili kuingia mzunguko wa pili wakiwa na alama zote 45 mikononi mwao.
Kibarua cha Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) Mbali na kutawala Ligi Kuu ya Tanzania, Simba SC inajiandaa na vita nyingine nzito katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League). Katika kundi lao, Simba itachuana vikali na miamba ya soka barani Afrika ikiwamo Orlando Pirates (Afrika Kusini), RS Berkane (Morocco), na Colombe (Cameroon).