Habari za Michezo
Habari za michezo

HII HAPA TIMU YA AFRIKA WANAOTAKA KUMPA AJIRA YA UKOCHA MOURINHO….

admin March 26, 2024 7:27 pm

Majadiliano kati ya Kocha kutoka nchini Ureno Jose Mourinho na Shirikisho la Soka nchini Cameroon ‘FECAFOOT’ yanaonekana kupiga hatua kubwa kwa ajili ya kocha huyo kuinoa ‘The Indomitable Lion’.

Cameroon imekuwa katika mchakato wa kumsaka Kocha Mkuu wa Mpya wa Kikosi chao cha Taifa, baada ya kuachana na Kocha mzawa Rigobert Song mwezi uliopita.

José Mourinho anatafuta changamoto mpya baada ya kuachana na klabu ya AS Roma ya Italia Januari 2024, kufuatia mfululizo mbaya wa matokeo ligi kuu Italia.

‘The Special One’ anaweza kuchukua mikoba ya kuinoa timu ya taifa ya Cameroon endapo mazungumzo yatakwenda vizuri na Cameroon.

Ingawa Mourinho anapewa nafasi kubwa ya kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa mshahara unaweza kuwa kikwazo kati yake na Cameroon.

KUELEKEA MECHI vs MAMELOD….KOCHA SIMBA AINGILIA KATI…AWAPA MBINU ZA USHINDI YANGA… KUELEKEA MECHI vs AL AHLY….ONANA AKUMBUSHIA ALIVYOWAFANYA WYDAD KWA MKAPA….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply