Habari za Simba leo
Habari za michezo

KUELEKA MECHI vs AL AHLY KESHO…TRY AGAIN ATUPA ‘FUPA’ LA LAWAMA KWA MASTAA SIMBA…

admin April 4, 2024 3:47 pm

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya Simba, Salim Abdullah ‘Try Again’ amewatoa hofu mashabiki waliokata tamaa baada ya kupoteza mchezo wa kwanza wa robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly uliochezwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, Machi 29, 2024

Try Again amesema nafasi ya timu hiyo kufuzu nusu fainali ya michuano hiyo bado ipo kwani wana dakika nyingine 90 za kupambana na kupata matokeo mazuri.

“Sisi tupo mawindoni, hatuwezi kukata tamaa ndio maana kuna mchezo wa kwanza na wa pili, tuna nafasi nyingine ya kupambana na tumejiandaa vizuri.”

Ameongeza kuwa, wachezaji wamepewa motisha kubwa ili kuongeza morali ya kupambana kupata matokeo mazuri.

“Tumewapa motisha kubwa, Rais wa Heshima, Mohamed Dewji ameweka motisha kubwa ambayo haijawahi kutokea, nisingependa kuweka wazi, wachezaji washindwe wenyewe.”

Try Again amesafiri na timu kwenda Cairo kwaajili ya mchezo wa pili wa robo fainali ya CAFCL utakaochezwa April 5, 2024 kwenye uwanja wa kimataifa wa Cairo saa 5:00 Usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

MASTAA SIMBA KUMWAGIWA MIL 812 KUZITOA MAMELOD NA AL AHLY….MABOSI WACHARUKA… HII HAPA 5 HOT STRIKE YA MERIDIANBET CASINO…HAPA MKWANJA NI UHAKIKA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply