Habari za Yanga leo
Habari za michezo

GAMONDI:- SIJAIANDAA YANGA KUCHEZA NA MAMELOD….KILICHOTOKEA MSIMU ULIOPITA MLIKIONA…

admin April 5, 2024 4:27 pm

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema kuwa timu yake imekwenda Afrika Kusini kwa lengo moja tu la kutafuta ushindi na kufuzu kwenda nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na si vinginevyo.

Gamondi amesema hayo jana Alhamisi Machi 4, 2024 wakati akizungumza kwenye mkutano na wanahabari kuelekea mchezo wa robo fainali ya michuano hiyo dhidi ya Mamelodi Sundowns utakaopigwa kesho nchini humo.

“Utakuwa mchezo mgumu lakini ni lazima baada ya dakika 90 kuwe na mshindi mmoja. Mpaka sasa mchezo uko 50/50 bado kila timu ina nafasi hivyo tuko hapa kuhakikisha tunapambana kupata matokeo mazuri.

“Siwaandai wachezaji wangu kwa ajili ya historia ya Mamelodi, naandaa timu yangu kutokana na dakika 90 zinazokuja. Tunaamini kazi tuliyofanya kwenye Uwanja wa mazoezi, tuna imani na wachezaji na Mashabiki wetu, haitakuwa rahisi kwetu na kwao pia.

“Tuna Wachezaji wenye uzoefu wenye sifa ya kupambana, msimu uliopita kwenye Fainali ya Kombe la Shirikisho walipoteza nyumbani lakini wote mnajua kilichotokea walipokwenda ugenini, kesho (leo) ni mchezo tofauti lakini watapambana tena kwa ajili ya mashabiki wetu,” amesema Miguel Gamondi.

DAUDA:- YANGA WAKIKAZA KIDOGO TU WANATOBOA LEO…ILA SIMBA MHHHH CHAMA NA AZIZ KI WALIVYOMALIZA MICHUANO YA CAF KIBABE…REKODI ZAO NI BALAA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply