Habari za Yanga leo
Habari za michezo

KUELEKEA MECHI vs MAMELOD LEO….ENG HERSI AANIKA GHARAMA ZA YANGA KUKAA SAUZI…

admin April 5, 2024 3:55 pm

Rais wa Klabu ya Yanga Engineer Hersi Said ameeleza gharama ya safari ya timu hiyo kwenda Afrika Kusini kwenye mechi klabu bingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns itakayochezwa leo Ijumaa.

Hersi akiongea na chama cha waandishi habari wa Afrika Kusini (SAFJA) amesema safari yao inagharimu Dola za Kimarekani 80,000 (Tsh Milioni 206)

“Ni gharama sana kuendesha klabu ya mpira wa miguu. Ninaweza kukuambia safari yetu kuja Afrika Kusini kucheza na Mamelodi inagharimu USD 80,000” — Amesema Hersi

“Tiketi ya kwenda na kurudi (kwa mtu mmoja) ni USD 600. Na nimekuja na watu 50. Hiyo ni USD 30,000. Watu 50 mara USD 150 kwa siku, zidisha kwa siku nne. Hiyo ni USD 30,000 nyingine.

“Hapo hujanunua kitu chochote na gharama za hoteli. Unatakiwa kuzunguka hapa na pale. Baadhi ya wachezaji na benchi la ufundi wanatakiwa kupewa posho wanaposafiri.

KUHUSU TATIZO LA MASTRAIKA SIMBA….MAYELE AJIPIGIA DEBE KIAINA…’LOLOTE LINAWEZA KUTOKEA..’ HII HAPA SLOT  MPYA YA KUVUNA MIHELA NDANI YA MERIDIANBET CASINO….ANZA LEO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply