Habari za Simba leo
Habari za michezo

MBINU HII INAYOTUMIWA NA TFF DHIDI YA SIMBA NA YANGA…YATUMIWA KWA PSG YA UFARANSA..

Marce Ben Komba April 22, 2024 6:16 pm

Kumekuwa na utaratibu au kawaida ya mechi mbalimbali kusogezwa mbele au kubadilishwa kwa ratiba ili kuzipa muda wa maandalizi zaidi Simba na Yanga kwenye mechi za CAF

Msimu huu pia kabla ya Yanga kucheza na Mamelodi sundowns pamoja na Simba kucheza na Al Ahly robo fainali za klabu bingwa hilo pia lilitokea kwa kusogezwa mbele au kubadilishwa ratiba ili kuwapa maandakizi mazuri kwa Simba na Yanga kuziendea mechi hizo muhimu

Kama ulijua ni Afrika pekee hayo huwa yanatokea basi huenda taarifa ya PSG kutocheza mechi mbili za ligi ili kujianda na mechi za nusu fainali ligi ya mabingwa dhidi ya Borussia Dortmund zitakupa kitu kuhusu umuhimu wa mashirikisho kuzipa muda wa maandalizi timu zao kwenye michezo muhimu

Mechi ya April 27 dhidi ya Le Havre na ile May 4 dhidi ya Nice zote zimeahirishwa ili kupisha michezo miwili ya nusu fainali dhidi ya Dortmund zitakazochezwa April 30 pamoja ule mchezo wa marejeano utakaopigwa May 7

GUEDE AANZA MBWEMBWE YANGA…BAADA YA KUIFUNGA SIMBA…AMEFUNGUKA HAYA KISA AZIZ KI NA CHAMA…AZAM KUZIMWAGIA MAMILIONI YA PESA SIMBA, YANGA….