Habari za Michezo leo
Habari za michezo

USAJILI HUU SIMBA HAWAACHI KITU AISEE…MASHINE HII KUTOKA AZAM NAYO YATUA UNYAMANI…

admin July 17, 2024 7:57 am

UONGOZI wa klabu ya Simba unaendelea kuimarisha kikosi chao hii ni baada ya kukamilisha usajili wa kinda kutoka timu ya vijana chini ya miaka 20 (U-20) ya Azam FC, Mohamoud Haji.

Wakati Haji akiwa na timu ya vijana ya Azam FC, kwenye mechi 19 alizocheza amefunga mabao 11 kati ya hayo ana hat-trick moja ana ametoa pasi tatu za mwisho zilizozaa mabao.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Simba kimesema kuwa wana imani kubwa na kinda huyo kutokana na kuwa na jicho la kuona goli huku kikiweka wazi kuwa watamtumia kwenye kikosi cha timu ya vijana.

“Ni kweli tumekamilisha usajili wa mshambuliaji huyo kwa mkataba wa miaka miwili lakini nafikiri ataanzia timu ya vijana kabla ya kupandishwa timu ya wakubwa lakini ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa wa kuona goli,” kilisema chanzo hicho.

KUHUSU NANI ATAANZA KATI YA PACOME, CHAMA NA AZIZI KI…JIBU LA GAMONDI HILI HAPA…. HUKUMU YA YANGA YAZUA BALAA…MAGOMA AFUNGUKA URAIS WA HERSI