habari za simba-Mabululu
Habari za Simba Leo

MTU WA KUCHUNGWA ZAIDI AL AHLI VS SIMBA.

Abubakar September 11, 2024 9:47 am

MNYAMA Simba inatakiwa kuwa makini sana na mshambuliaji wa Tripoli, Agostinho Cristóvão Paciência, maarufu kama Mabululu ambaye amekuwa akiitumikia timu ya Taifa ya Angola kutokana na kiwango cha juu na uzoefu ambao amekuwa nao kwenye michuano ya kimataifa Afrika.

Mabululu ambaye ameshazichezea timu kadhaa kubwa Afrika kama Al Ittihad ya Misri, Petro de Luanda na Libolo, ameshacheza timu ya Taifa ya Angola michezo 36 na kufunga mabao 12 akiwa kati ya wachezaji waliocheza michezo michache na kufunga mabao mengi kwenye timu hiyo.

Kocha wa Simba Fadlu Davids, alisema wamejiandaa vizuri kuwakabili Al Ahli Tripoli wakiwa wamekamilisha sehemu kubwa ya maandalizi yao.

“Al Ahli Tripoli ni timu nzuri na imekuwa na historia ya kufanya vizuri kwenye mashindano haya huko nyuma. Hata hivyo, sisi ni timu kubwa naamini tunaweza kufanya mambo makubwa kwenye mchezo huu wa Jumapili ijayo.”

SIMBA YAWAFUATA AL AHLI…MAMBO MATATU YA FAIDA KWAO FEI TOTO ANA BALAA  HUYO…MUDATHIR AWAPIGIA SIMU GUINEA