Home Habari za michezo TETESI ZA USAJILI LEO:- MASHINE HII YA KAZI YANUKIA YANGA….YONDANI NAYE ATAJWA….

TETESI ZA USAJILI LEO:- MASHINE HII YA KAZI YANUKIA YANGA….YONDANI NAYE ATAJWA….

Tetesi za Usajili leo

Dirisha dogo la usajili Tanzania

litafunguliwa Dec 16 hadi January 15, hivyo vyota kama Elie Mpanzu, ataanza kuitumikia Simba Dec 18 dhidi ya Ken Gold.

Yes! Mhanga wa kwanza ni Ken Gold 😃

———————————

Yanga wako kwenye mazungumzo ya mwisho na klabu ya Singida Black Stars, ili kuinasa saini ya kiungo Kelvin Nashon (24) kwa Mkopo.

Yanga wanamtaka Kelvin Nashon kwa mkopo wa miezi (6) na Singida wako tayari kumuachia hivyo dirisha dogo likifunguliwa kiungo huyo atatua jangwani.


Baada ya mkongwe Kelvin Yondani kumalizana na Pamba Jiji sasa ni zamu ya Deus Kaseke ‘Mwaisa Mtu Mbadi’ ambaye pia amejiunga na timu hiyo tayari kwa ajili ya kuongeza nguvu kikosini humo.

Wawili hao wameshawahi kucheza pamoja na wanaungana na timu hiyo wakiwa wachezaji huru baada ya kila mmoja kutoka timu tofauti, Yondani akitokea Geita Gold iliyoshuka daraja, wakati Kaseke alikuwa anaitumikia Fountaine Gate (zamani Singida Fountain Gate).

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Pamba kimenieleza kuwa, kiungo huyo tayari ameungana na timu na anaendelea na mazoezi kujiweka tayari kwa ushindani mara baada ya dirisha dogo kufunguliwa.

—————————–

SOMA NA HII  IWE JUA IWE MVUA SIMBA AJA NA KAULI NGUMU DHIDI YA POWER DYNAMO