Habari za michezo

YANGA NA SIMBA WAUNGANA SAFARI YAO MOJA

Vardo February 15, 2026 9:34 pm

USICHEKE mamba kabla hujavuka mto! Methali hii inaonekana kuwakumba klabu ya Yanga  baada ya kile kilichotokea kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Wakati wengi wakiamini mambo yamekaa sawa, mwisho wa safari umeonyesha kuwa hakuna wa kumcheka mwenzake, wote wa hapa hapa.

Yanga  waliingia katika mchezo wao wa mwisho wakiwa na presha kubwa ya kutafuta ushindi mnono huku macho yao yakitazama matokeo ya mchezo mwingine wa kundi hilo.

Wakicheza visiwani Zanzibar, walionyesha dhamira ya kweli kwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0, ushindi uliowapa matumaini makubwa ya kusonga mbele.

Mabao ya Yanga yalifungwa na nyota wao Laurindo Dilson Maria Aurélio ‘Depu’ dakika ya 35 na 64, kabla ya Chadrack Boka kuongeza bao la tatu dakika ya 66 na kuzima kabisa upinzani wa wapinzani wao.

Ilikuwa ni burudani tosha kwa mashabiki waliokuwa wamefurika uwanjani wakiamini ndoto ya robo fainali iko mlangoni.

Hata hivyo, furaha hiyo haikudumu kwa muda mrefu. Matokeo ya mchezo mwingine kati ya Al Ahly SC na AS FAR Rabat hayakwenda kama walivyotarajia Wananchi.

Sare ya Al Ahly na Far Rabat yasiyowapa faida Yanga yaliwafanya wabaki nafasi ya tatu kwenye kundi hilo wakiwa na alama nane.

Al Ahly waliongoza kundi kwa alama 10 huku AS FAR Rabat wakishika nafasi ya pili kwa pointi tisa, na timu hizo mbili ndizo zilizofanikiwa kutinga hatua ya robo fainali, Yanga, licha ya kupambana hadi dakika ya mwisho, walijikuta wakigonga mwamba.

Matokeo hayo yanamaanisha kuwa Yanga wanaungana na watani zao, Simba  kuaga michuano hiyo katika hatua ya makundi. Hivyo basi, kejeli na vijembe vinabaki kuwa vya muda mfupi, kwani mwisho wa siku uwakilishi wa Tanzania umekomea hapo.

Soka lina matokeo yasiyotabirika. Leo unaweza kucheka, kesho ukalia. Ndiyo maana kauli ya “hakuna wa kumcheka mwenzake” inabeba uzito wake wote wa hapa hapa.

RUBY PLAY NA SABABU YA KUCHEZA KASINO MERIDIANBET ISHU YA PENALTI NAMUNGO IKO HIVI