Home Habari za michezo EXPANSE STUDIOS YAUNGANISHA NGUVU NA STAKE KUKUZA SOKO LA MICHEZO YA KUBAHATISHA

EXPANSE STUDIOS YAUNGANISHA NGUVU NA STAKE KUKUZA SOKO LA MICHEZO YA KUBAHATISHA

0

Soko la kimataifa la michezo ya kubahatisha linaendelea kupata msisimko zaidi baada ya Expanse Studios kutangaza rasmi ushirikiano mpya na jukwaa maarufu la ubashiri duniani, Stake. Hatua hii ni sehemu ya mkakati wa kupanua usambazaji wa michezo yao kwa wachezaji wengi zaidi duniani, huku ikiimarisha nafasi ya Expanse kama mmoja wa wabunifu wakubwa wa michezo ya kubahatisha.

Kwa muda sasa, Expanse Studios imekuwa ikitengeneza michezo inayovutia na yenye ubunifu wa hali ya juu. Majina kama Super Heli, Wild Icy Fruits, na VASO Psycho yamekuwa gumzo katika majukwaa ya ubashiri duniani kwa sababu ya muundo wake wa kisasa na burudani yake isiyotabirika. Kuanzia sasa, wachezaji wa Stake sasa wataweza kufurahia michezo hii maarufu.

Expanse Studios ni sehemu ya kundi kubwa la Meridian Holdings Inc., ambao wanamiliki na kuendesha kampuni kadhaa zenye mafanikio makubwa katika sekta ya michezo na burudani. Ndani yake pia kuna Meridianbet Group inayofanya kazi katika nchi nyingi duniani, pamoja na RKings nchini Uingereza, Mexplay nchini Mexico na Classics for a Cause nchini Australia.

Akizungumza kuhusu hatua hiyo, Mtendaji Mkuu wa Expanse Studios, Damjan Stamenkovic, alisema ushirikiano huo ni ishara ya ukuaji mkubwa wa kampuni hiyo. Alibainisha kuwa Stake ni chapa yenye ushawishi mkubwa katika tasnia ya michezo ya kubahatisha duniani, na kupitia mtandao wa Hub88, michezo ya Expanse sasa itawafikia wachezaji wengi zaidi.

Ikiwa na zaidi ya washirika 1,300 duniani pamoja na mkusanyiko wa zaidi ya michezo 70 ya kipekee, Expanse Studios inaendelea kujenga historia mpya katika tasnia ya michezo ya kubahatisha. Ushirikiano huu na Stake unaonesha wazi dhamira ya kampuni hiyo ya kuendelea kusukuma mipaka ya ubunifu, kuimarisha upatikanaji wa michezo yake duniani.