Home Habari za michezo DEPU AREJEA, YANGA YAMPA MPANGO MAALUM KABLA YA KARIAKOO DERBY

DEPU AREJEA, YANGA YAMPA MPANGO MAALUM KABLA YA KARIAKOO DERBY

0

MSHAMBULIAJI wa Yanga SC, Laurindo Dilson Maria Aurélio ‘Depu’, amerejea tena kwenye mazoezi ya timu baada ya kupona majeraha yaliyokuwa yamekuwa yakimuweka nje ya uwanja kwa muda.

Depu ameonekana akiwa na hali nzuri zaidi ya utimamu wa mwili, hatua inayotoa matumaini kwa benchi la ufundi la Yanga kuelekea michezo muhimu inayowakabili katika ratiba ya msimu huu.

Nyota huyo anatarajiwa kutumika katika michuano ya Kombe la Muungano kama sehemu ya mpango maalum wa kumrejesha taratibu kwenye kiwango chake bora, kabla ya mechi kubwa ya Kariakoo Derby dhidi ya Simba.

Kocha Mkuu wa Yanga, Pedro Gonçalves, ameweka wazi mpango wa kumtumia Depu kwa tahadhari, akilenga kuhakikisha anapata muda wa kutosha wa kurejesha utimamu wake wa mwili na kuimarisha morali ya ushambuliaji wa timu.

Michuano hiyo ya Muungano itakuwa fursa muhimu kwa Yanga kumtengeneza upya mshambuliaji huyo, ili awe katika ubora unaotakiwa wakati watakapokutana na wapinzani wao wakubwa, Simba, Mei 3, 2026.

Yanga inaamini kurejea kwa Depu kutaleta chachu mpya kwenye safu yao ya ushambuliaji katika kipindi hiki muhimu cha msimu.