Nyumba yake ya Manchester iko katika eneo la kifahari yenye thamani ya Pauni 11 milioni, huku pia akiwa na nyingine Barcelona, Hispania, katika eneo la Pedralbes, ambalo ni la matajiri linalokadiriwa kuwa na thamani Pauni 7 milioni.
MISAADA KWA JAMII
Kocha huyu hajisahau linapokuja suala la kusaidia jamii. Amechangia fedha katika sekta ya afya, hasa wakati wa janga la COVID-19 nchini Hispania. Pia amekuwa akisaidia miradi ya watoto na elimu.
Zaidi ya hapo, Guardiola amekuwa akitoa sauti yake katika masuala ya kijamii na haki za binadamu, akionesha kuwa mafanikio yake hayaishii uwanjani pekee.
MAISHA YA FAMILIA
Guardiola na Cristina Serra walifunga ndoa mwaka 2014 baada ya kuwa pamoja kwa zaidi ya miaka 20 na walikutana wakiwa vijana, Pep akiwa na miaka 18 na wana watoto watatu: Maria, Màrius na Valentina.
Kwa mujibu wa taarifa za hivi karibuni, Pep na Cristina walitengana mwaka 2024/2025 baada ya kuwa pamoja kwa zaidi ya miaka 30, ingawa wanaendelea kuwa na mahusiano mazuri kwa ajili ya familia yao.