“Ana Ofa nyingi sana ila kwa sasa atakachokiangalia ni pesa kwanza na sio kingine. Kwa hiyo hata kama timu ipo India ila ina pesa kuwazidi wote waliomuwekea ofa, ataenda,” kimesema chanzo hicho.
Uhamisho wa Clara kutoka Dux Lugrono ya Hispania kwenda Al Nassr uligharimu kiasi cha Sh51 milioni ya usajili, lakini mshahara wake ndani ya misimu mitatu, mwaka wa kwanza alikunja sh19 milioni, mwaka jana alilipwa sh23 milioni na mwaka huu analipwa sh27 milioni.