Azam FC

AZAM YAMFUATA STAA SERENGETI BOYS

Vardo June 1, 2026 9:06 pm

AZAM FC imeanza mchakato wa kumuwania mshambuliaji wa Serengeti Boys na Kagera Sugar, Luqman Ali, kwa ajili ya msimu ujao.

Luqman ameendelea kung’ara katika michuano ya Afrika kwa vijana, ambapo alifunga penati ya ushindi iliyoiondoa Misri kwenye hatua ya nusu fainali.

Kutokana na kiwango chake, kocha wa Taifa Stars, Miguel Gamondi amemjumuisha kwenye kikosi cha timu ya taifa kwa mechi za kalenda ya Fifa dhidi ya Uganda na Rwanda.

Taarifa za ndani zinaeleza Azam tayari imewasiliana na Kagera Sugar kujadili uwezekano wa kumpata mshambuliaji huyo.

“Tunafurahishwa na kiwango chake. Ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa na tuna matarajio makubwa naye,” alisema mmoja wa viongozi wa Kagera Sugar.

“Ni kweli kuna timu nyingi zimeonyesha nia ya kumtaka, ikiwamo Azam, lakini kwa sasa hatujafikia hatua ya kufanya maamuzi kuhusu kumuuza.” Fainali ya kihistoria ya Serengeti Boys dhidi ya Senegal inatarajiwa kuchezwa leo Juni 2, 2026, saa 4:00 usiku.

KOMBE LA DUNIA LAICHEZESHA SIMBA MCHANA USHINDI UNAOKUJA KWA KASI YA MWANGA