Azam FC

FEI TOTO ACHOMOLEWA STARS, MAJERAHA YATAJWA

Vardo June 1, 2026 2:18 pm

KIUNGO mshambuliaji wa Taifa Stars, Feisal Salum ‘Fei Toto’ ameondolewa katika kikosi cha timu hiyo kinachojiandaa na mechi mbili za kirafiki za kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), dhidi ya Uganda na Rwanda baada ya kupata majeraha.

Akizungumza na Soka la Bongo, Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Cliford Ndimbo amesema licha ya mchezaji huyo kuitwa katika kikosi hicho ila amegundulika na majeraha ambayo yamemuondoa rasmi kikosini humo.

“Baada ya Fei Toto kuwasili kambini alionekana hayuko fiti na alipofanyiwa uchunguzi zaidi jopo la matatibu limeona hatoweza kucheza mechi hizo mbili za kirafiki,” amesema Ndimbo.

Aidha, Ndimbo amesema licha ya Fei Toto kutokuwa sehemu ya timu hiyo, ila hakuna mchezaji aliyeongezwa hadi sasa kwa ajili ya kuzipa nafasi yake, japo ikitokea wataweka wazi.

Katika hatua nyingine, Ndimbo amesema timu ya Tanzania itaondoka leo saa 5:00 usiku kwenda Morocco kwa ajili ya mechi mbili za kirafiki dhidi ya Uganda ‘The Cranes’ Juni 5, kisha kupambana na Rwanda ‘Amavubi’ Juni 9.

HAKUNA KIZUIZI, SIMBA QUEENS WAJIKUSANYIA MATAJI NA KUANDIKA HISTORIA MPYA MASTAA STARS WAPANIA AFCON 2027