MAIGAN, AC MILAN NGOMA NGUMU, CHELSEA IKITAJWA KUMVIZIA
KIPA wa kimataifa wa Ufaransa na AC Milan, Mike Maignan, inadaiwa kuwasilisha ombi la kuondoka kikosini kutokana na mwisho mbaya wa msimu wa timu yake kulikoenda sambamba na kufutwa kazi kwa kocha Massimiliano Allegri.
Inadaiwa Maigman ambaye amekuwa nahodha wa AC Milan kwa muda mrefu amewekewa mzigo mezani na Chelsea ambao wako tayari kufufua harakati zao za kumsajili.
Kwa mujibu wa Calciomercato, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 aliyeongoza mkataba mwanzoni mwa mwaka huu hadi Juni 30, 2031, amebadilisha mawazo ya kubaki Milan muda mrefu akidaiwa kufikiria zaidi ofa ya Chelsea na timu zingine kubwa za Ulaya ambazo hazitajwi zilizoomba kumsajili.
Maigman ambaye ni mmoja wa mastaa wenye mafanikio makubwa Milan tangu alipotua Julai Mosi, 2021 akitokea Lille ya Ufaransa, pia anadaiwa kuanza kugomea simu za mabosi wanaotaka kuzungumza naye sasa akiwa na kikosi katika Ufaransa kinachojiaandaa kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia 2026.
DUSAN Vlahovic anapanga kufanya duru ya mwisho ya mazungumzo na Juventus kuhusu mkataba mpya kabla ya mkataba wake wa sasa kumalizika mwisho wa mwezi huu na anataka kubaki Turin, lakini atazingatia ofa kutoka Chelsea na Newcastle United iwapo makubaliano hayatapatikana.
Tayari uongozi wa Juventus umeshaonyesha hofu juu ya makubaliano kwani nyota huyo anataka mshahara mkubwa ambao hawawezi kumlipa.
Marc Casado
KIUNGO Marc Casado yupo karibu kuondoka Barcelona kwenda AS Monaco anakotakiwa msimu ujao na hiyo inatokana na kuanza kupoteza nafasi katika kikosi cha kwanza cha mabingwa wa Ligi Kuu Hispania (La Liga).
Mbali na Monaco, kuna klabu kadhaa za England ikiwemo Aston Villa, Brighton, Crystal Palace, Everton, Manchester United, Newcastle na Nottingham Forest, zimeshafanya mazungumzo na kambi yake, lakini hazikuendelea zaidi.
Darwin Nunez
STRAIKA wa kimataifa wa Uruguay, Darwin Nunez anatarajia kurejea Liverpool msimu ujao ikiwa mkataba wake na Al Hilal ya Saudi Arabia utavunjwa kama inavyotarajiwa.
Hata hivyo, kurejea Anfield hakuchukuliwi jambo linalowezekana sana ingawa kuna taarifa zinazomhusisha na chama lake hilo la zamani. Inaelezwa Chelsea na Newcastle United zote zinamwania mchezaji huyo.
Rayan Vitor
LIVERPOOL inaonekana kuwa sehemu inayowezekana kutua mshambuliaji wa Bournemouth, Rayan Vitor kufuatia uteuzi wa kocha wa zamani wa Bournemouth, Andoni Iraola ambaye ameshajiunga na kikosi hicho.
Hata hivyo, uhamisho huo utawezekana kuanzia Januari mwakani wakati kipengele cha kuachiliwa kwa Pauni 130 milioni kitakapoanza kufanya kazi na huenda kikapungua zaidi siku zijazo.
Sam Johnstone
MANCHESTER United wanaangalia uwezekano wa kumsajili tena kipa Sam Johnstone kutoka Wolverhampton Wanderers, ambapo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 aliyewahi kupita akademi ya United, anapendelea uhamisho huo kwa sababu za kifamilia. Johnstone anaichezea Wolves ambayo tayari imeshashuka Ligi Kuu England.
Morgan Gibbs-White
ARSENAL inamuona kiungo Nottingham Forest, Morgan Gibbs-White, kama mbadala wa sahihi wa Morgan Rogers wa Aston Villa, ambaye anawindwa na Paris Saint-Germain.
Rogers amekuwa katika rada ya timu mbalimbali Ulaya na anahusishwa kwenye mazungumzo ya kutua ama Hispania au Italia. Hata hivyo, nguvu kubwa ipo timu za England.
Raoul Bellanova
BEKI na winga wa kulia wa kimataifa wa Italia na Atalanta, Raoul Bellanova, 26, anadaiwa kuwekwa sokoni msimu huu na mabosi wa kikosi hicho wanapambana kusaka fedha kwa ajili ya usajili.
Atalanta wanawasiliana kwa sasa na Nottingham Forest pamoja na Tottenham Hotspur zilizoonyesha nia ya kumchukua. Thamani ya nyota huyo ni takriban Pauni 17 milioni.