Habari za michezo

REFA MSOMALIA ALIYEZUIWA MAREKANI KUCHEZESHA UEFA SUPER CUP

Vardo June 11, 2026 8:38 pm

Umoja wa Vyama vya Mpira wa Miguu Ulaya (UEFA) umempanga Refa Omar Artan kuchezesha mechi ya taji la UEFA Super 2026 baina ya PSG na Aston Villa, Agosti 12, 2026.

Taarifa hiyo imetolewa leo Alhamisi, Juni 11, 2026 ikiwa ni siku nne tangu Artan alipozuiliwa kuingia Marekani kwa ajili ya kuchezesha Fainali za Kombe la Dunia zinazoanza leo.

Serikali ya Marekani ilidai kwamba ilimzuia Artan kwa sababu za kiusalama huku baadaye Shrikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) likitangaza kwamba Refa huyo hatochezesha tena mashindano hayo.

RAYVANNY AKIWASHA KOMBE LA DUNIA MASTAA WAWAPA SALUTI, OKELLO,BARKER KUNYAKUA TUZO ZA NBC