Yanga SC

YANGA YAMALIZA KAZI KWA AZIZ KI, AL ITTIHAD YAKUBALI OFA

Vardo June 25, 2026 5:33 pm

DILI la kurejea kwa kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki ndani ya kikosi cha Yanga limeingia hatua za mwisho baada ya klabu yake ya sasa, Al-Ittihad, kuridhishwa na ofa iliyowasilishwa na mabingwa hao wa Tanzania.

Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali zinaeleza kuwa Aziz Ki mwenyewe ameonyesha nia ya kuondoka Al-Ittihad mwishoni mwa msimu huu ili kurejea Yanga, klabu aliyowahi kuitumikia kwa mafanikio makubwa na kujijengea heshima kubwa ndani na nje ya Tanzania.

Inaelezwa kuwa Yanga imewasilisha ofa yenye thamani ya dola za Marekani 350,000 kwa ajili ya kupata huduma za nyota huyo, ambaye bado ana nafasi ya kipekee mioyoni mwa mashabiki wa timu hiyo kutokana na mchango wake mkubwa alipokuwa akivaa jezi za Wananchi.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, viongozi wa Al-Ittihad wanaendelea kuifanyia kazi ofa hiyo huku wakifikiria kumruhusu mchezaji huyo kuondoka, hasa kutokana na hamu yake ya kurejea katika mazingira aliyowahi kung’ara na kupata mafanikio makubwa.

Kurejea kwa Aziz Ki kutakuwa moja ya usajili mkubwa zaidi wa Yanga katika dirisha hili, huku klabu hiyo ikiendelea kujenga kikosi imara kwa ajili ya kutetea mafanikio yake ya ndani na kufanya vizuri zaidi katika michuano ya kimataifa msimu ujao.

MSIMBAZI WAMUWINDA MSHAMBULIAJI ALIYETIKISA AFRIKA