Yanga SC

SIRI NZITO YAENDELEA KUWATESA, KAMWE ASEMA NENO…………….

Vardo June 27, 2026 10:18 am

KADRI mchezo wa Yanga dhidi ya TRA United unavyozidi kusogea, ndivyo hali ya sintofahamu kuhusu ujumbe ambao viongozi wa klabu hiyo wamekuwa wakiutoa inavyoendelea kutawala miongoni mwa mashabiki na wadau wa soka.

Wengi wameendelea kujiuliza Yanga inaandaa tangazo gani kubwa, huku Afisa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Ally Kamwe, amesisitiza kuwa majibu yote yatapatikana mara baada ya mchezo huo wa leo.

Yanga unashuka dimbani leo kuwakaribisha TRA United katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania utakaopigwa uwanja wa KMC Complex, Mwege Dar es Salaam.

 

Kamwe amesema kwa siku kadhaa kumekuwa na tafsiri mbalimbali kuhusu kauli ambazo zimekuwa zikitolewa na viongozi wa Yanga, lakini nyingi ya tafsiri hizo zimekuwa tofauti na ujumbe halisi ambao klabu inalenga kuufikisha.

Amesisitiza kuwa hakuna haja ya kukimbilia hitimisho, kwani kila kitu kitawekwa wazi baada ya mchezo dhidi ya TRA United, huku akiwataka mashabiki kuendelea kuwa na subira.

“Kama tulivyosema kuelekea mechi yetu na TRA, yeyote anayefuatilia bado kuna mengi hajayaelewa. Waendelee kufuatilia tu, ya kushangaza yapo mengi yanakuja. Kama hawajaelewa leo baada ya mchezo dhidi ya TRA United wataelewa,” amesema Kamwe.

Kauli hiyo imeendelea kuzua mjadala mkubwa katika mitandao ya kijamii na miongoni mwa wadau wa soka, ambapo wengi wameanza kubashiri kuwa Yanga huenda inajiandaa kutangaza jambo kubwa litakalovuta hisia za mashabiki wake.

Hata hivyo, Kamwe hakufafanua ni jambo gani hasa litakalowekwa wazi, hatua ambayo imezidi kuongeza hamasa na matarajio kuelekea pambano hilo muhimu.

Macho na masikio ya mashabiki wa soka yameelekezwa kwenye mchezo wa leo, wakisubiri kuona kama Yanga itatimiza ahadi yake ya kufichua siri ambayo imekuwa ikiidokeza kupitia kauli za viongozi wake kwa siku kadhaa zilizopita.

NDAIRAGIJE AJIAMINI KABLA YA YANGA, POINTI 42 ZINATUTOSHA……. CHIPO NA HESABU KALI LIGI KUU BARA