UBELGIJI YATINGA 32 BORA YAONGOZA KUNDI G
VANCOUVER, CANADA: USHINDI wa mabao 5-1 ilioupata Ubelgiji kwenye mechi ya kundi G, umeifanya timu hiyo ifuzu hatua ya 32 bora ya Kombe la Dunia ikikusanya pointi tano na kukaa kileleni. Imeungana na Misri iliyomaliza ya pili na pointi tano pia.
Nyota aliyefungua akaunti ya mabao kwa Ubelgiji alikuwa Leandro Trossard aliyefunga mawili dakika ya 28 na 50 akitumia vizuri makosa ya safu ya ulinzi ya New Zealand na kuthibitisha ubora wake mbele ya lango.
Timu hiyo iliendelea kutengeneza mashambulizi na dakika ya 66, Kevin De Bruyne aliiandikia bao la tatu timu hiyo kabla ya New Zealand kufunga bao pekee dakika ya 84 likiwekwa kambani na Elijah Just.
Kwa matokeo hayo yanaifanya New Zealand kumaliza mkiani na pointi moja kwenye mechi tatu za makundi ambapo timu hiyo haijapata ushindi ikitoka sare moja na kupoteza mbili. Nafasi ya tatu ikishikwa na Iran yenye pointi tatu.
ILIVYOKUWA
Takwimu zinaonyesha kipindi cha kwanza Ubelgiji ilikuwa na asilimia 52 za kumiliki mpira dhidi ya 48 za New Zealand, lakini tofauti kubwa ilikuwa kwenye mashambulizi ambapo ilijaribu mashuti 23 huku wapinzani wao wakipiga matatu pekee.
Hilo lilionyesha namna safu ya ushambuliaji ya Ubelgiji ilivyokuwa bora kwenye kushambulia lango la wapinzani.
Ndani ya kipindi hicho hali ilikuwa mbaya zaidi kwa New Zealand, Ubelgiji ilimaliza dakika 45 ikipiga mashuti 15 dhidi ya sifuri ya wapinzani wao na ikitengeneza nafasi nne zilizolenga lango.
Licha ya New Zealand kujaribu kujitutumua kupitia Elijah Just katika kipindi cha pili, juhudi zilikwamishwa na kipa wa Ubelgiji, Thibaut Courtois aliyekuwa imara langoni.