SOKA LA KIZAMANI LIMERUDI KIBABE KOMBE LA DUNIA 2026…..?
KUNA mengi yanaendelea katika fainali za Kombe la Dunia 2026 ambako kuna rekodi kibao zinavunjwa na zingine hazijavunja hadi sasa. Lakini, wakati nchi zilizofuzu mtoano wa hatua ya 32 bora zikijifua kwa ajili ya michuano hiyo, kuna jambo jingine limeibuka. Nalo ni namna mpira unavyochezwa sasa licha ya maendeleo makubwa yaliyofikiwa katika mchezo huo kiuchezaji.
Lakini, je, uchezaji wa kale wa mipira ya pembeni unarudi katika Kombe la Dunia 2026? Kimsingi fainali hizi zimeshuhudia idadi kubwa ya mabao yakitokana na mipira ya krosi, lakini hilo halimaanishi kuwa mashambulizi ya mipira ya juu ndiyo njia pekee ya mafanikio.
Upana au ukubwa wa uwanja, krosi nyingi kuelekea katika boksi, na winga wa jadi (yaani wachezaji wa kulia kucheza kulia na wa kushoto kucheza kushoto) wanaoshikilia mistari ya pembeni mara nyingi hii huitwa wchezaji wa kale wa pembeni , na kauli hiyo huleta picha fulani kuhusu jinsi inavyotazamwa katika baadhi ya mitazamo.
Lakini, tunaposema kila mara kuwa soka ni la mzunguko humaanisha kwamba mitindo huja na kuondoka, na katika Kombe la Dunia 2026, uchezaji wa pembeni umechukua nafasi muhimu. Kwa uhalisia, hatuwezi kuweka kila kitu tulichokiona katika kundi la “uchezaji wa kale wa pembeni†kwa sababu bado kuna mawinga wengi wa kisasa wanaocheza upande usio wa mguu wao wenye nguvu.
Hata hivyo, unaweza kuwa umegundua kuwa wachezaji wa pembeni wanachangia sana mafanikio ya timu nyingi katika michuano hii ya majira ya joto, kwa mtindo wa kitamaduni zaidi badala ya kukata kuelekea ndani na kupiga mashuti.
Iwe ni winga, ‘wing-back’ au mabeki wa pembeni wanaopanda kushambulia, tunaona mabao mengi yakitokana na krosi zinazoingia boksi kutoka pembeni. Timu 29 kati ya 48 zilizofuzu katika mashindano ya Kombe la Dunia 2026 zimefunga angalau bao moja ndani ya sekunde tano baada ya krosi kuingia kwenye boksi.
UHOLANZI INAONGOZA
Uholanzi ndiyo wanaoongoza kwa hilo na walifunga kupitia krosi katika mechi mbili za kwanza za makundi. Kwanza kulikuwa na bao la kichwa la kuvutia la Virgil van Dijk dhidi ya Japan kupitia krosi ya Ryan Gravenberch; kisha katika ushindi mkubwa dhidi ya Sweden, Brian Brobbey alifunga mabao mawili kutokana na krosi za chini, na Cody Gakpo alifunga bao la nyuma ya lango kupitia krosi ya Denzel Dumfries.
Ureno pia ni miongoni mwa timu zilizofunga mabao manne ndani ya sekunde tano baada ya krosi, matatu yakiwa ni dhidi ya Uzbekistan, ikiwemo bao la Cristiano Ronaldo kutokana na krosi ya Joao Cancelo.
Norway nao wamefaidika na mtindo huu, wakifunga mabao matatu dhidi ya Irak kupitia krosi. Bao lao la kwanza lilikuwa mfano wa mabao yaliyotrendi katika michuano hiyo ambapo krosi ya chini ilipita nyuma ya safu ya ulinzi na Erling Haaland alikuwa mfungaji katika tukio hilo, akiingiza mpira langoni
Wengine walionufaika na mabao kama hayo ni Lamine Yamal (Hispania), Gakpo na Brobbey (Uholanzi), pamoja na bao la kujifunga la Mohamed Hany wa Misri dhidi ya Ubelgiji lililotokana na krosi ya Thomas Meunier wa Ubelgiji.
Tukirejea nyuma hadi Kombe la Dunia 1966, ni fainali za 2002 zilizopigwa Japan na Korea ndizo pekee zilizozidi wastani huo, zikiwa na wastani wa 0.84 kwa kila mechi. Hivyo 2026 iko karibu sana na rekodi hiyo, huku Kombe la Dunia 2022 lilikuwa na wastani wa wastani wa 0.55, hivyo kuna ongezeko la takriban asilimia 36.4.
Mipira ya kona pia ina mchango mkubwa, ikiwa na wastani wa mabao 0.36 kwa kila mechi ikiwa ni moja ya viwango vya juu zaidi kwenye historia ya Kombe la Dunia. Sababu nyingine inaweza kuwa teknolojia ya VAR na mfumo wa kuamua offside kwa usahihi zaidi, unaosaidia wachezaji wanaokimbilia kupokea krosi wasikamatwe kimakosa.
Lakini, pia inawezekana timu zinatafuta njia za moja kwa moja kuvunja mabeki wanaojilinda kwa idadi kubwa nyuma. Mfano ni Canada dhidi ya Qatar, ambapo walipiga krosi 55 ikiwa ni miongoni mwa idadi kubwa zaidi kwenye historia ya Kombe la Dunia.
Qatar walicheza kwa kujilinda zaidi, hivyo Canada walilazimika kutumia mipira ya pembeni mara kwa mara, na mkakati huo uliwasaidia kupata mabao. Kwa ujumla, asilimia 33.3 ya mabao ya mashindano hayo yametokana na krosi au sekunde tano baada ya krosi karibu theluthi moja.
Hata hivyo, siyo kila mara mkakati huo unafanya kazi. Timu zinapopiga krosi nyingi katika mechi moja, mara nyingi hazishindi. Hii inaonyesha kuwa mafanikio yanategemea mchanganyiko wa ubunifu, muda sahihi wa kutumia pembeni, na wachezaji wenye uwezo wa kutoa krosi sahihi.
Au huenda ni suala la mzunguko wa bahati tu kwa sasa. Kombe la Dunia 2026 linaonyesha dalili za kurudi kwa ladha ya “uchezaji wa kale wa pembeni†, lakini bado mapema kusema kuwa mtindo huo umerudi rasmi au ni mwenendo wa muda tu.