Simba SC

Simba Sc Yafafanua Mkakati Wake wa Mwisho Msimu Huu

Vardo June 28, 2026 1:25 pm

UONGOZI wa Simba SC umeweka wazi kuwa kwa sasa haujajiingiza katika mashindano ya moja kwa moja na klabu nyingine yoyote kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara, ukisisitiza kuwa kipaumbele chao kikubwa ni kukamilisha ratiba ya michezo iliyobaki kwa nidhamu na heshima.

 

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amesema klabu hiyo imekuwa na msimamo thabiti tangu mwanzo wa msimu kuhusu malengo yao, ambayo ni kuhakikisha wanamaliza michezo yao yote kwa ushindi na kufanya tathmini baada ya ligi kumalizika.

 

“Hatushindani na yoyote, sisi tunapambana kumaliza Ligi Kuu Tanzania Bara, na malengo tuliyojiwekea ni kumaliza michezo yetu yote iliyopo mkononi kwa ushindi.

 

Tuliweka wazi hili tangu kwenye kampeni yetu, tukiwa na michezo mitano tulilenga kumaliza ligi kwa kushinda, na bado tunaendelea na hilo.

Baada ya kumaliza ligi tutafanya tathmini yetu, kisha suala la usajili litafuata.
Hatukimbizani na timu yoyote zaidi ya kukamilisha ratiba kwa heshima. Baada ya hapo tutaangalia tulikosea wapi, nani ametufikisha hapa tulipo, nani ametukwamisha, na wapi tulipokwama. Baada ya hapo tutarekebisha na kuelekea msimu ujao,” amesema Ahmed.

Kauli hiyo imekuja kama ujumbe wa utulivu kutoka kambini kwa Simba, ikionyesha kuwa kwa sasa macho yao yote yapo kwenye kumaliza msimu kabla ya kuanza mipango mipya ya kikosi kuelekea msimu ujao.

Ndoto Zinakua Mali Halisi Ukicheza Meridianbet Bonanza Canada, Afrika Kusini Katika Vita ya Kihistoria Hatua ya 32