Meridianbet Yaandika Hadithi Mpya Ya Matumaini Kwa Wasichana Katavi
Katika kona mbalimbali za Tanzania, kuna wasichana wenye ndoto kubwa za kuwa madaktari, walimu, wahandisi na viongozi wa kesho. Hata hivyo, baadhi yao hukumbana na changamoto ambazo huonekana ndogo kwa wengine lakini zenye athari kubwa katika maisha yao. Meridianbet, kupitia programu zake za Uwajibikaji kwa Jamii, imeamua kusimama pamoja na wasichana hao kwa kutoa msaada wa taulo za kike ili kuunga mkono kampeni ya Hedhi Salama katika kata ya Kasekese, Manispaa ya Wilaya ya Tanganyika.
Msaada huu umetokana na uelewa kwamba afya na elimu ni nguzo muhimu za maendeleo ya jamii. Meridianbet inaamini kuwa msichana anapopata mazingira bora ya kujisitiri na kujitunza, anakuwa na uwezo mkubwa wa kushiriki kikamilifu katika masomo na shughuli za maendeleo. Kupitia msaada huu, kampuni hiyo imeonyesha kuwa sekta binafsi inaweza kuwa mshirika muhimu katika kutatua changamoto zinazowakabili vijana na kujenga jamii yenye usawa zaidi.
Meridianbet haikuachi nyuma, kuna michezo mbalimbali ya kasino mtandaoni pamoja na mechi za kimataifa za kubashiri zenye odds bomba na nafasi ya kuongeza kipato chako kila siku. Kujiunga ni rahisi! Tembelea tovuti ya MERIDIANBET au piga *149*10#.
Viongozi wa Kata ya Kasekese wakiongozwa na Afisa Mtendaji wa Kata hiyo, Bi. Bahati Kasanga wameeleza kuwa msaada huo umewafikia wasichana wengi ambao walihitaji msaada huo kwa kiwango kikubwa. Wamepongeza Meridianbet kwa kuonyesha mfano wa uwajibikaji kwa jamii unaolenga matokeo halisi. Kwa mujibu wao, msaada huo utachangia kuboresha afya, kuongeza mahudhurio ya shule na kujenga kujiamini kwa wasichana wengi ambao ni sehemu muhimu ya maendeleo ya taifa.
Kwa miaka ya hivi karibuni, Meridianbet imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya kijamii inayolenga kugusa maisha ya wananchi moja kwa moja. Kampuni hiyo inaamini kuwa mafanikio ya biashara yanapaswa kuambatana na mchango kwa jamii. Ndiyo maana miradi yake ya CSR imekuwa ikilenga maeneo yenye mahitaji makubwa, huku ikitoa kipaumbele kwa afya, elimu na ustawi wa vijana.
Msaada huu kwa mabinti wa kata ya Kasekese ni mfano halisi wa jinsi mshikamano unavyoweza kubadilisha maisha. Meridianbet inaendelea kuamini kuwa kila hatua ya kusaidia jamii ni uwekezaji katika kesho yenye matumaini zaidi. Kwa kuwapa wasichana nafasi ya kuendelea na masomo yao kwa kujiamini, kampuni hiyo imeendelea kuandika historia ya uwajibikaji kwa jamii inayogusa mioyo na kubadilisha maisha.