Michezo Bongo

Kabunda, Mfuko Wajisogeza Mashujaa

Vardo July 14, 2026 7:40 pm

TIMU ya Mashujaa iliyomaliza msimu wa 2025-2026 ikiwa nafasi ya 11 na pointi 33 katika Ligi Kuu Bara, imeanza kukifanyia marekebisho kikosi chake huku tetesi zikidai kuwa timu hiyo inasajili wachezaji watakaongeza nguvu ya ushindani kwa msimu ujao.

Miongoni mwa wachezaji wanaotajwa kumalizana na timu hiyo ni kiungo mshambuliaji Hassan Kabunda na beki wa kati, Abdallah Mfuko wote kutoka Namungo.

Watu wa karibu na wachezaji hao wamesema tayari timu ya Mashujaa imemalizana nao, hivyo ni suala la muda kutambulishwa kwa mashabiki wa timu hiyo.

“Kila kitu kimekamilika, imebakia tu kwa viongozi kuwatangaza mbele ya mashabiki wao, uzoefu wao wameona utaisaidia timu hiyo kumaliza nafasi za juu zaidi kwenye msimamo wa ligi tofauti na uliyopita,” kimesema chanzo hicho.

Alipotafutwa Mfuko amesema: “Siwezi kuzungumzia chochote kuhusiana na usajili wa nitacheza wapi, itafika muda sahihi kila mtu atajua nitakuwa na timu gani.”

Alipotafutwa meneja wa Mashujaa, Athuman Athuman ili kuthibitisha hilo amesema: “Nipo kijijini kwetu siwezi kujua ishu za usajili kwa sasa, hivyo sina cha kukwambia kuhusiana na jambo hilo nikiwa nje ya kazi labda nikisharudi kuungana na timu nitakwambia.”

Simba Yamng’ang’ania Kasali, Barker Atoa Sababu Ya Kumbakiza France na Spain Wakutana Kwenye Mbio za Ufalme wa Soka