Jermain Defoe Woking FC
Habari za michezo

Jermain Defoe Ajiuzulu Ghafla Ukocha Woking FC Baada ya Miezi 4 Pekee!

Vardo July 24, 2026 5:59 pm

Nyota wa zamani wa timu ya taifa ya England, Jermain Defoe, ametangaza kuondoka katika klabu ya Woking FC inayoshiriki Ligi ya National League nchini Uingereza, baada ya kudumu madarakani kwa miezi minne pekee.

Defoe, ambaye alikuwa tayari yupo kwenye maandalizi ya kikosi hicho kwa ajili ya msimu mpya, aliongoza mechi sita pekee rasmi kabla ya kufanya maamuzi hayo ya ghafla ya kujiuzulu.

Mgogoro wa Ndani Watajwa

Kwa mujibu wa taarifa kutoka nchini Uingereza, Defoe hakutokea kuendesha mazoezi ya timu hiyo siku ya Alhamisi na badaye aliipigia simu uongozi wa klabu kuwajulisha uamuzi wake wa kuachia ngazi.

Vyanzo vya karibu vinaeleza kuwa kulikuwa na sintofahamu na mgogoro wa ndani kati ya Defoe na mmoja wa viongozi wa juu wa Woking FC, ingawa klabu hiyo imekataa kuweka wazi maelezo zaidi kuhusu suala hilo. Katika mechi sita alizofundisha, Defoe alipoteza mchezo mmoja pekee na kuifanya timu hiyo kumaliza katika nafasi ya 10 kwenye msimamo wa ligi.

Taarifa Rasmi ya Woking FC

Kupitia taarifa yao rasmi kwa umma, klabu ya Woking ilisema:

“Woking Football Club inathibitisha kuwa klabu na kocha wa timu ya kwanza, Jermain Defoe, wamekubaliana kuachana mara moja. Tunamshukuru kwa mchango wake na tunamtakia kila la heri katika hatua zake za baadaye.”

Defoe Funguka Sababu ya Kuondoka

Naye Defoe, kupitia ukurasa wake wa Instagram, aliandika ujumbe wa kuaga na kueleza kusikitishwa kwake na namna safari hiyo ilivyoishia njiani:

Baada ya mazungumzo ya hivi karibuni, ninaweza kuthibitisha kuwa nimekubaliana na Woking kuondoka katika nafasi yangu ya ukocha. Kwa bahati mbaya, mazingira yaliyopo yamefanya isiwezekane kuendelea.  

Najivunia kazi tuliyoifanya na niliamini tulikuwa tunajenga kitu maalumu. Nawashukuru viongozi, mashabiki na zaidi wachezaji ambao ninawaonea huruma kwa sababu ni kundi bora sana.  

Nimevunjika moyo kuona safari imefika mwisho mapema, lakini ninaondoka nikiwa na fahari kubwa kwa kile tulichokuwa tunakijenga. Uzoefu wangu Woking utanifanya kuwa kocha imara zaidi katika hatua inayofuata ya maisha yangu.”  

UFC YAPOKEA UDHAMINI MKUBWA KUTOKA MERIDIANBET Juma Shaaban James Aachana na KVZ: Vita Nzito Ya Saini Yake Yaiva Zanzibar!