Barker aonya Simba SC
Simba SC

Barker Aonya Simba SC: “Bado Hatujamaliza Kazi!” Yaahidi Vita Dar

Vardo September 8, 2026 8:32 am

Klabu ya Simba SC imerejea nchini ikitokea Malawi huku ikiwa na tabasamu la ushindi, lakini Kocha Mkuu Steve Barker amegoma kulevya na matokeo hayo, akisisitiza kuwa Wekundu wa Msimbazi hawatakiwi kubweteka hata kidogo na faida ya bao moja waliyopata ugenini dhidi ya Mighty Wanderers.

Ushindi huo wa ugenini katika mchezo wa kwanza wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika umeiweka Simba kwenye nafasi nzuri ya kutinga hatua inayofuata. Hata hivyo, Barker ametuma ujumbe mzito kwa wachezaji na mashabiki akibainisha kuwa kibarua bado ni kizito kuelekea mchezo wa marudiano unaotarajiwa kuwa na presha kubwa.

Simba sasa imehamishia nguvu zote kwenye maandalizi ya pambano hilo la marudiano litakalopigwa Jumapili, Septemba 13, 2026, katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Wapinzani Hawaji Kutalii

Akitathmini mchezo huo, Barker amesema ushindi wa ugenini ulikuwa mwanzo mzuri wa safari yao kimataifa, lakini amewataka wachezaji wake kubaki na umakini wa hali ya juu kwani Mighty Wanderers wana uwezo na mpango wa kuja kupindua meza.

“Safari yetu ya Ligi ya Mabingwa Afrika ilianza juzi kwa ushindi ugenini. Sasa, tunaandaa mchezo unaofuata,” amesema Barker.

Kocha huyo ameongeza kuwa wanatakiwa kutumia vyema muda uliopo kujiandaa kisaikolojia na kiufundi, akitambua kwamba wapinzani wao hawatakuja Dar es Salaam kwa ajili ya kutalii, bali kupambana kufa na kupona ili kugeuza matokeo.

Kwa upande wa Simba SC, hesabu ni moja tu: kutumia faida ya bao la ugenini, nguvu ya mashabiki, na ukuta wa nyumbani kuhakikisha wanatamatisha kazi na kukata tiketi ya hatua inayofuata.

Irene Uwoya Afunguka Kutokea Bodi ya Filamu: “Tunaitambua A-List Yetu Tu” Steve Barker Athibitisha Libasse Gueye Kuiva Simba SC vs Mighty Wanderers