Cristiano Ronaldo na Georgina Rodriguez
Habari za michezo

Cristiano Ronaldo na Georgina Rodriguez Funga Ndoa? Wanawake 7 Aliowahi Kutoka Nao

Vardo August 5, 2026 8:43 am

LISBON, URENO: Supastaa wa soka duniani, Cristiano Ronaldo, anaripotiwa kuingia kwenye hatua mpya ya maisha baada ya kuenea kwa taarifa kuwa huenda akafunga ndoa hivi karibuni na mchumba wake wa siku nyingi, Georgina Rodriguez.

Wawili hawa wamekuwa pamoja tangu mwaka 2016 baada ya kukutana katika duka la kifahari la Gucci jijini Madrid, Hispania. Kwa sasa, Ronaldo na Georgina wanasimamia familia yenye watoto watano: Cristiano Jr, Mateo, Eva Maria, Alana Martina, na Bella Esmeralda.

Uvumi wa harusi yao ulipamba moto baada ya Georgina kuonyesha pete kubwa ya almasi aliyovishwa. Ingawa tarehe rasmi haijatangazwa, taarifa za ndani zinaeleza kuwa sherehe hiyo huenda ikafanyika katika eneo la kihistoria la Quinta da Regaleira kule Sintra, Ureno.

Hata hivyo, kabla ya kutulia thabiti na Georgina, mshambuliaji huyo wa zamani wa Real Madrid na Manchester United alipitia kwenye mahusiano na wanawake kadhaa maarufu duniani. Hapa kuna orodha ya wanawake 7 waliowahi kuhusishwa kimapenzi na CR7:


1. Imogen Thomas (2006)

Mwaka 2006, Ronaldo alihusishwa na aliyekuwa mshiriki wa shindano la Big Brother, Imogen Thomas. Wawili hawa walikutana wakati CR7 akiwa anaichezea Manchester United. Licha ya uvumi kurudi tena mwaka 2011, wote wawili walikanusha kuwa kwenye mahusiano ya kina.

2. Gemma Atkinson (2007)

Mwigizaji wa Uingereza, Gemma Atkinson, alikuwa kwenye uhusiano na Ronaldo kwa takribani miezi minne. Gemma aliwahi kuweka wazi kuwa mzozo wao wa kwanza wa kimahusiano ulihusisha Ronaldo kumwalika nyumbani kwake kunywa chai na kutazama vipindi vya vichekesho.

3. Bipasha Basu (2007)

Baadaye mwaka 2007, Ronaldo alionekana akiwa katika wakati wa mahaba na nyota wa filamu za Bollywood, Bipasha Basu, kwenye klabu ya usiku mjini Lisbon. Inasemekana ukaribu tao ulitokana na mapenzi ya Ronaldo kwa filamu za Kihindi.

4. Paris Hilton (2009)

Baada ya kuhamia Real Madrid mwaka 2009, Ronaldo alionekana mara kadhaa akijirusha na mrithi wa familia ya Hilton, Paris Hilton, jijini Los Angeles, Marekani. Uhusiano wao ulikuwa wa muda mfupi sana kabla ya Paris kueleza kuwa walibaki kuwa marafiki wa kawaida.

5. Kim Kardashian (2010)

Mwaka 2010, mfanyabiashara na nyota wa vipindi vya televisheni, Kim Kardashian, alionekana jijini Madrid akipata chakula cha jioni na Ronaldo. Wawili hao walitumia siku chache pamoja kabla ya kila mmoja kuendelea na maisha yake.

6. Irina Shayk (2010 – 2015)

Kabla ya Georgina, mwanamitindo wa kimataifa kutoka Urusi, Irina Shayk, ndiye aliyedumu muda mrefu zaidi na Ronaldo. Walikutana kwenye mradi wa matangazo ya mitindo na kudumu kwa miaka mitano. Walichumbiana mwaka 2011 lakini walitengana mwaka 2015 kabla ya kufunga ndoa.

7. Desiree Cordero (2016)

Muda mfupi kabla ya kukutana na Georgina, Ronaldo alikuwa kwenye mahusiano ya muda mfupi na aliyewahi kuwa Miss Spain 2014, Desiree Cordero. Hata hivyo, walitengana kutokana na kutofautiana mtazamo wa malengo yao ya baadaye.


Mwisho wa Tofauti, Mwanzo wa Familia

Baada ya mabadiliko na changamoto nyingi za kimahusiano, Cristiano Ronaldo hatimaye alipata utulivu kwa Georgina Rodriguez. Kwa sasa, familia hiyo inaendelea kufurahia maisha na likizo kwenye visiwa mbalimbali duniani kama Mallorca, huku mashabiki wakisubiri kwa hamu siku ya harusi yao ya kihistoria.

Neo Maema Ametua Simba SC! Rejea Yake Msimbazi Yatikisa Uhamisho Ligi Kuu Rayon Sports Yaitinga Fainali CECAFA Kagame Cup 2026 baada ya Kuichapa Jamus SC