Prichard Colon afariki dunia
Habari za michezo

Bondia Prichard Colón Afariki Dunia Akiwa na Umri wa Miaka 33 Baada ya Miaka 11 ya Ulemavu

Vardo August 14, 2026 11:10 pm

BONDIA mashuhuri kutoka Puerto Rico, Prichard Colón, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 33, Alhamisi ya Agosti 13, 2026. Taarifa za msiba huu mzito zamethibitishwa na baba yake mzazi, Richard Colón, kupitia ujumbe wa majazi kwenye mitandao ya kijamii.

Colón ameaga dunia baada ya kuishi kwa takribani miaka 11 akisumbuliwa na ulemavu mkubwa wa ubongo—jeraha lililotokana na pambano lake la kihistoria dhidi ya Terrell Williams lililofanyika Oktoba 17, 2015, huko Virginia, Marekani. Katika pambano hilo, Colón alipigwa mfululizo ngumi haramu za kisogoni (rabbit punches).

Muda mfupi baada ya kurudi chumba cha kubadilishia nguo, Colón alianza kutapika kisha kuanguka ghafla. Vipimo vya madaktari vilionyesha alipata uvujaji mkubwa wa damu kwenye ubongo, hali iliyolazimu afanyiwe upasuaji wa dharura. Alikaa kwenye koma kwa siku 221 (zaidi ya miezi saba).

Hata alipozinduka, maisha yake hayakuwa sawa tena. Colón alipoteza uwezo wa kutembea, kuzungumza, na kujihudumia mwenyewe, na kulazimika kutegemea uangalizi wa karibu wa wazazi wake kwa kipindi chote hicho.

Kabla ya mkasa huo, Colón alitabiriwa kuwa nyota mkubwa wa ngumi duniani. Akiwa na umri wa miaka 23 pekee, alikuwa hajapoteza pambano hata moja, akiwa na rekodi ya ushindi wa michezo 16 mfululizo, ambapo 13 kati ya hayo alishinda kwa KO.

Shinda TSh Milioni 6! Mashindano ya Expanse Epic Spins Meridianbet Baraket Hmidi Aondoka Azam FC, Rejea Stade Tunisien