Usajili wa Mlandege FC: Mlandelge Yashusha Mitambo Mipya ya Vijana 2026/27
BAADA ya kufanya usafi wa kikosi kwa kuachana na wachezaji 15, klabu ya Mlandege imeanza rasmi mchakato wa kusajili mitambo mipya kuelekea msimu wa 2026/2027, ikilenga kujenga timu yenye mchanganyiko wa damu changa na ushindani wa muda mrefu.
Katika usajili wa msimu huu, Mlandege imeweka nguvu kubwa kwa wachezaji wenye umri wa chini ya miaka 20. Miongoni mwa sura mpya zilizotambulishwa ni pamoja na:
-
Said Seif Said (17): Winga wa kulia kutoka Small Simba.
-
Amiri Zaid Ali (20): Beki wa kati kutoka Annour Academy.
-
Ramadhan Juma (17): Beki wa pembeni kutoka Dulla Sunday.
-
Abdul Nassa Michuz (18): Mshambuliaji hatari kutoka Inter Zanzibar.
-
Muhammed Mustafa (16): Kiungo mshambuliaji kutoka TMS International Arusha.
-
Aver Terlumun Paul (18): Kiungo wa kati kutoka Flight Football Club (Nigeria).
-
Mabrouk Ame Fundi (19): Kiungo namba kumi kutoka Wawi.
-
Fahad Hafidh Mohammed (23): Kiungo mkabaji kutoka Fufuni.
-
Abdallah Jumanne Said (19): Beki imara kutoka JKU.
Akizungumzia mwelekeo huo mpya, Katibu Mkuu wa Mlandege, Hussein Ahmada, ameeleza kuwa maamuzi ya kusajili vijana yanajenga msingi wa timu kudumu kwa muda mrefu na kucheza soka la ushindani wa juu.
Amesisitiza kuwa wachezaji vijana wana uwezo mkubwa wa kufundishwa, kuelewa mbinu haraka, na kukaa klabuni kwa muda mrefu tofauti na wachezaji wakongwe.