Benchi la ufundi Yanga
Yanga SC

Yanga Yaongeza Nguvu Benchi la Ufundi: Ekotto Ajiunga Rasmi Kutoka ZNZ

Vardo August 18, 2026 9:28 am

KLABU ya Yanga imeendelea kuweka mambo sawa katika benchi lake la ufundi baada ya kufanya usajili mwingine wa kocha wa viungo, Abdulwahid Abdallah ‘Ekotto’, ambaye anakwenda kuungana na Tshephang Mokaila ‘Chyna’.

Ekotto, ambaye si mgeni katika soka la Bongo kwani alishawahi kufanya kazi na klabu za KMC FC pamoja na Mlandege FC ya Zanzibar, amejiunga na Wananchi ili kuongeza nguvu zaidi kwenye eneo la utimamu wa mwili chini ya Kocha Mkuu, Manqoba Mngqithi.

Kocha huyo mzawa anaungana na Mbotswana, Chyna, ambaye yupo kikosini hapo kwa msimu wake wa pili mtawalia tangu alipojiunga akitokea AmaZulu FC ya Afrika Kusini.

Ujio wa Ekotto unaifanya Yanga sasa kuwa na jumla ya wataalamu saba (7) kwenye benchi lao la ufundi linaloongozwa na Kocha Mkuu Manqoba Mngqithi, aliyejiunga na timu hiyo Julai 10, 2026, akitokea Golden Arrows FC.

Wanaounda Benchi la Ufundi la Yanga Sasa:

  • Kocha Mkuu: Manqoba Mngqithi (Afrika Kusini)

  • Kocha Msaidizi: Simo Dladla (Afrika Kusini)

  • Kocha wa Makipa: Greg Etafia (Nigeria)

  • Makocha wa Viungo (Fitness): Tshephang Mokaila ‘Chyna’ (Botswana) & Abdulwahid Abdallah ‘Ekotto’ (Tanzania)

  • Kocha wa Mipira ya Kutenga (Set-piece): Kagisho Dikgacoi (Afrika Kusini)

  • Mtathmini Mchezo (Video Analyst): Yardaan Valodia (Afrika Kusini)

Uongozi wa Yanga umeamua kuongeza nguvu kwenye eneo la utimamu wa mwili ili kuwapunguzia wachezaji ugumu na uchovu wa ratiba, ikizingatiwa kuwa timu hiyo inakabiliwa na michezo mingi ya ushindani ikiwemo Ligi Kuu Bara ambapo wameanza kampeni ya kutetea taji lao la 31.

Peter Shalulile Afichua Siri ya Ushindi Yanga SC Rekodi Zawabeba Mashujaa, Namungo Ligi Kuu Bara Leo