Ibrahim Jabaar Aomba Radhi Simba SC Baada ya Kadi Nyekundu Dhidi ya Pamba Jiji
KIUNGO machachari wa Simba SC, Ibrahim Jabaar, ameonyesha kiwango cha juu cha ukomavu na profeshenali baada ya kukubali kuwajibika kikamilifu kufuatia kadi nyekundu aliyoonyeshwa katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Pamba Jiji.
Jabaar alionyeshwa kadi hiyo nyekundu katika mchezo mkali uliopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, hatua iliyomlazimisha kuiacha timu yake ikicheza ikiwa na mchezaji pungufu uwanjani.
Baada ya mshtuko wa tukio hilo, kiungo huyo hakutafuta sababu wala visingizio. Kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Instagram, Jabaar aliandika ujumbe mzito uliowagusa mashabiki wengi wa Simba:
βHakuna visingizio. Ninachukua jukumu kamili.β
Kauli hiyo imepokelewa vyema na wanasoka wengi, ikionyesha utayari wake wa kujifunza kutokana na makosa na kurejea akiwa bora zaidi.
Mchezaji huyo, ambaye ni nguzo muhimu katika safu ya kiungo ya Simba msimu huu, sasa anaiangazia michezo ijayo kwa umakini zaidi ili kuisaidia timu yake kupata matokeo chanya kwenye mbio za ubingwa.