Mbosso na WCB Wasafi
Burudani

Mbosso na WCB Wasafi: Rekodi za Youtube za Lava Lava na D Voice

Vardo August 22, 2026 5:55 pm

Kutokana na ustadi na ushawishi wake, Mbosso amekuwa nguzo muhimu katika mafanikio ya kibiashara ya wasanii wenzake wa lebo hiyo, akionyesha uwezo wa kuwavuta mashabiki wengi kupitia nyimbo za kushirikiana.

Ushawishi wa Mbosso kwa Lava Lava Wimbo uliofanya vizuri zaidi kwenye mtandao wa YouTube kwa msanii Lava Lava ni “Basi Tu” (2021), ambao amemshirikisha Mbosso. Video ya wimbo huo iliyoongozwa na Director Kenny imeshatazamwa mara milioni 30.2, ikiwa ndiyo kazi yake yenye namba za juu zaidi kwenye mtandao huo na kuipiku ngoma yake ya kwanza ya “Tuachane” (2017).

Mbosso na D Voice: Mfano wa Singeli na Bongofleva

Licha ya D Voice kufanya kazi na wasanii wakubwa kama Diamond Platnumz na Zuchu, wimbo wake unaoongoza kwa kutazamwa zaidi YouTube ni “Tunapendana” (2024) alioshirikiana na Mbosso. Wimbo huo wa miondoko ya Singeli umepata tazama zaidi ya milioni 36.2, ukiipiku miungano yake na Zuchu kama “BamBam”, “Nani”, na “Baridi”.

Rekodi Zilizopo na Uwezo wa Mbosso

  • Lava Lava: Wimbo wa “Basi Tu” uliopata views mil 30.2 ndio namba moja yake.

  • D Voice: Wimbo wa “Tunapendana” wenye views mil 36.2 ndio namba moja yake.

  • Zuchu: Bado anashikilia rekodi ya msanii wa kwanza solo Afrika Mashariki kufikisha views milioni 100 kupitia wimbo wa “Sukari”.

Baada ya kuondoka WCB na kuanzisha lebo yake ya Khan Music, Mbosso anaendelea kuonyesha kuwa mchango wake kwenye nyimbo za kushirikiana unaleta matokeo makubwa ya kibiashara kwenye Bongofleva.

Si Msaada Pekee, Meridianbet Yafika Tabata Kisukuru kwa Upendo Thomas Gravesen: Makubwa ya ‘Mad Dog’ Aliyemng’oa Jino Ronaldo na Kutisha Real Madrid