Bernardo Silva Real Madrid
Habari za michezo

Bernardo Silva na Ines Tomaz: Maisha Mapya Real Madrid na Mipango ya Familia

Vardo August 29, 2026 7:20 pm

Msimu wa kwanza wa Bernardo Silva (31) ndani ya klabu ya Real Madrid unagusa pia maisha yake ya familia. Bernardo na mkewe Ines Tomaz (28), mwanamitindo mwenye ndoto kubwa, wameingia mwaka wa tatu wa ndoa yao huku wakianza maisha mapya nchini Hispania.

Kiungo huyo wa kimataifa wa Ureno alijiunga na Real Madrid kama mchezaji huru akitokea Manchester City, klabu aliyoitumikia kwa miaka tisa na kupata mafanikio makubwa kwa kushinda takribani kila taji la klabu.

Kutoka Manchester Hadi Santiago Bernabeu

Kabla ya kutua Real Madrid chini ya Kocha Jose Mourinho, Bernardo alihusishwa na klabu kadhaa ikiwemo Atletico Madrid, Juventus, na Barcelona.

Wawili hao walifunga ndoa Julai 1, 2023, katika sherehe iliyofanyika kwenye bonde la Douro nchini Ureno. Mwezi mmoja baadaye, Agosti 2023, walipata mtoto wao wa kwanza wa kike, Carlota.

Mipango ya Familia Kubwa

Katika mahojiano na mtandao wa HELLO!, Bernardo alieleza jinsi kuzaliwa kwa Carlota kulivyobadilisha mtindo wa maisha yao:

“Sasa hivi kila kitu ninachofanya kinalenga kumfurahisha Carlota. Mimi na Ines hatuna tena muda wa kukaa peke wetu, lakini ana tabia nzuri sana.”

Pia alisema wana mipango ya kukuza familia zao zaidi:

“Siku zote tulitaka kuwa na familia kubwa. Hatutaki kuishia mtoto wa pili, bila shaka tutapata mtoto wa tatu na pengine wa nne baadaye.”

Kwa sasa, familia hiyo inayojiandaa kupokea mtoto wa pili imeanza rasmi maisha mapya jijini Madrid, ikiwa ni mwanzo wa ukurasa mwingine kwenye maisha ya Bernardo Silva akiwa mchezaji wa Real Madrid.

Usisubiri Mpaka Mwisho, Milioni 5 Ipo Dimbani Rumani za Usajili: Rashford Awindwa na Barcelona, Dili za Kean na Palacios Zawa Moto!