Dortmund vs Paderborn
Meridianbet

Nani kuibuka m’babe? Dortmund Kuikaribisha Paderborn

Vardo September 12, 2026 12:21 pm

Borussia Dortmund itakuwa mwenyeji wa SC Paderborn katika mchezo wa Bundesliga utakaopigwa leo Jumamosi, Septemba 12, 2026, katika Uwanja wa Signal Iduna Park. Mchezo huo utaanza saa 16:30 jioni, huku Dortmund ikilenga kuendelea na mwanzo wake mzuri wa msimu huu.

 

Dortmund imeanza msimu kwa ushindi katika michezo yake miwili ya kwanza, ikishinda Hamburger SV kwa mabao 2-0 kabla ya kuibuka na ushindi wa 3-2 dhidi ya Hoffenheim. Ushindi huo wa Hoffenheim ulikuwa muhimu zaidi baada ya timu hiyo kurejea kutoka nyuma na kuchukua pointi zote tatu.

 

Mshambuliaji Serhou Guirassy amekuwa miongoni mwa wachezaji muhimu wa Dortmund mwanzoni mwa msimu. Amefunga katika michezo yote miwili ya kwanza ya Bundesliga, hivyo Paderborn italazimika kuwa makini na safu ya ushambuliaji ya Dortmund.

 

Kwa upande wa Paderborn, timu hii bado inatafuta ushindi wake wa kwanza baada ya kupata sare ya 0-0 dhidi ya Mainz na kupoteza 1-0 dhidi ya Freiburg. Changamoto kubwa kwao imekuwa kwenye ufungaji, kwani hawajafunga bao katika michezo yao miwili ya kwanza ya ligi.

 

Meridianbet inasema kuna michezo kama Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli. Ingia katika kasino ya mtandaoni ya Meridianbet na ujiokotee mkwanja mapema.  Jiunge sasa au Tembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

 

Dortmund inaonekana kuwa na nafasi nzuri ya kuendeleza rekodi yake nzuri mbele ya mashabiki wake, lakini Paderborn inaweza kutumia mchezo huu kuonyesha ushindani baada ya kurejea Bundesliga. Hivyo, macho yatakuwa kwa Dortmund kuona kama itaendelea na kasi yake, huku wageni wakisaka matokeo yatakayowapa matumaini zaidi katika msimu huu.

Simba vs Mighty Wanderers: Ahadi ya Milioni 200 za MO Dewji Kuibeba Simba Kesho Uwanja wa Uhuru Burudani Yapanda Kiwango Kwa Uwepo Wa Play’n Go