Kassim Shaibu Mayele TRA United
Michezo Bongo

Mayele Wa TRA United Afunguka Ushindani Wa Namba, Aweka Wazi Lengo Lake Ligi Kuu

Vardo September 26, 2026 7:44 pm

MSHAMBULIAJI mpya wa TRA United, Kassim Shaibu maarufu kama ‘Mayele’, amefunguka kuhusu maendeleo yake klabuni hapo huku akikiri kukabiliwa na ushindani mkali wa namba kutoka kwa washambuliaji wenzake.

Mayele, aliyetua TRA United Julai 25, 2026 akitokea Mtibwa Sugar kwa mkataba wa miaka miwili, ameeza kuwa licha ya ugeni wake, anaendelea kuzoea mazingira na mfumo wa timu hiyo ili kutengeneza muunganiko bora na wenzake.

Akizungumza kuhusu nafasi yake kikosini, mshambuliaji huyo alisema:

“Kwa dakika chache ninazoendelea kuzipata, nataka nihakikishe nazitumia vizuri. Kwa sasa tuna benchi jipya la ufundi, hivyo ni wakati wa kila mchezaji kuonyesha kipaji chake ili kumshawishi kocha kupewa nafasi zaidi uwanjani.”

Licha ya kwamba hajafanikiwa kucheka na nyavu hadi sasa katika michezo ya Ligi Kuu Bara, Mayele amesisitiza kuwa hajakata tamaa kwani msimu bado ni mchanga na lengo lake kuu ni kuivunja rekodi yake ya msimu uliopita.

Katika msimu wa 2025-2026 akiwa na Mtibwa Sugar—ambayo ilishuka daraja baada ya kumaliza nafasi ya 15 na pointi 27—Mayele alihusika katika mabao matatu kati ya 25 ya timu hiyo, akifunga mabao mawili na kutoa asisti moja.

Pelican Yupo Tayari Kulipua Burudani Mpya Ya Kasino Mtandaoni Coastal Union Afichua Siri Baada ya Kukutana na Simba na Yanga