Kipa wa IAA SC
Michezo

Kipa wa IAA SC Aaron Kalambo: Ninaweza Kujiunga na Ligi Kuu Januari 2027

Vardo October 19, 2026 8:33 am

Kipa wa IAA SC ya Arusha, Aaron Kalambo, ameweka wazi kuwa licha ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja, bado ana mlango wazi wa kuondoka katika kikosi hicho ikiwa atapata timu inayocheza Ligi Kuu Bara kwenye dirisha dogo la usajili la Januari 2027.

Akizungumza na Soka La Bongo, Kalambo alibainisha kuwa mkataba wake una kipengele maalum kinachomruhusu kutimkia klabu ya Ligi Kuu Bara ifikapo Januari 2027, ingawa kwa sasa nguvu na malengo yake yote ni kupigania mafanikio ya kikosi hicho cha jijini Arusha.

“Malengo yangu ni kucheza Ligi Kuu, ndio maana kabla ya kusaini mkataba niliwaeleza viongozi jambo hili na kwa upande wao walinikubalia. Niliwaahidi kuwapigania ili kufanya vizuri kwenye Ligi ya Championship,” alisema Kalambo.

Kipa huyo, ambaye amewahi kuzipzea timu za Transit Camp, Coastal Union, Geita Gold, na Dodoma Jiji, anaamini kuwa uzoefu wake ni chachu kubwa ya kuisaidia IAA SC katika msimu wao wa kwanza wa Ligi ya Championship 2026-2027.

Hadi sasa, IAA SC inayoshiriki Championship kwa mara ya kwanza msimu huu, inashika nafasi ya 11 ikiwa na pointi 5 baada ya kucheza mechi tano (ushindi mmoja, sare mbili, na vipigo viwili). Timu hiyo ilipanda daraja kupitia mechi za ‘Play-Off’ kwa kuitoa African Sports ya Tanga kwa jumla ya mabao 3-2.

Siri ya Mafanikio ya Fatuma Issa ‘Fetty Densa’ Ndani ya Simba Queens Ben Starkie ATISHA Uingereza! Kizigo cha Mabao 4 Chaifanya Taifa Stars Kumulika