Ben Starkie
Michezo

Ben Starkie ATISHA Uingereza! Kizigo cha Mabao 4 Chaifanya Taifa Stars Kumulika

Vardo October 19, 2026 8:40 am

Kiungo mshambuliaji wa Tanzania, Ben Starkie, ameendelea kuwasha moto nchini Uingereza baada ya kuonyesha kiwango cha juu katika kikosi cha Truro City, timu anayoichezea kwa mkopo akitokea Harborough Town FC.

Starkie anaonekana kurejea kwenye ubora wake kamili baada ya kufunga mabao manne katika michezo mitatu ya mwisho aliyoanza katika kikosi cha kwanza. Kiwango hiki kinakuja baada ya kupitia kipindi kigumu msimu uliopita kutokana na majeraha yaliyomweka nje ya uwanja kwa muda mrefu.

Mabao haya yamerejesha matumaini makubwa kwa nyota huyo, huku yakimweka kwenye nafasi nzuri ya kuitwa tena katika kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars, chini ya Kocha Miguel Gamondi, ambaye amekuwa akifuatilia kwa karibu wachezaji wanaocheza nje ya mipaka ya Tanzania.

Starkie aliichezea Taifa Stars kwa mara ya kwanza mnamo Machi 24, 2022, kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati ambapo Tanzania ilishinda kwa mabao 3-1, na pia aliwahi kuwakilisha nchi katika kikosi cha vijana cha U-23 kwenye michezo ya kufuzu AFCON dhidi ya Sudan Kusini mnamo Septemba 2022.

Kipa wa IAA SC Aaron Kalambo: Ninaweza Kujiunga na Ligi Kuu Januari 2027 Wazazi Waliopinga Muziki: Safari ngumu ya Harmonize, Nandy na Davido kabla ya mafanikio