wasanii walivyopingwa na wazazi
Burudani

Wazazi Waliopinga Muziki: Safari ngumu ya Harmonize, Nandy na Davido kabla ya mafanikio

Vardo October 19, 2026 8:52 am

Sanaa ni mojawapo ya kazi zinazoingizia wasanii pesa nyingi na heshima duniani kutokana na vipaji vyao. Kwenye tasnia ya burudani na hasa muziki, vipaji vimekuwa vikiibuka kila kukicha, huku wasanii wakijitangaza ndani na nje ya mipaka ya mataifa yao.

Hakuna ubishi kwamba kila msanii anahitaji sapoti ya familia na mashabiki ili aanze, atoke, au azidi kukua kimuziki. Hata hivyo, safari haijawahi kuwa rahisi kwa wote. Wapo mastaa wakubwa ambao walitaka kukata tamaa kabisa kutokana na wazazi wao kushindwa kuwasapoti, wakiamini muziki si kazi yenye maisha ya baadaye na kuwataka wasome vitabu. Lakini baada ya kulazimisha na kupigania ndoto zao, wasanii hawa leo wamekuwa moto wa kuotea mbali!

Mastaa kama Harmonize, Nandy, Davido, Tyla, na wengine wengi hawakuachana na ndoto zao; walizipigania kwa jasho na damu, na sasa wanafaidi matunda ya vipaji vyao.

Ben Starkie ATISHA Uingereza! Kizigo cha Mabao 4 Chaifanya Taifa Stars Kumulika Ndoto ya Ndejembi: Simba na Yanga Zihamie Kwenye Basketball!