Wachezaji 10 Wanaolipwa Zaidi Duniani: Ronaldo Ashikilia Taji
LONDON, ENGLAND — Jarida maarufu la Forbes limetangaza rasmi orodha ya wachezaji wa soka wanaolipwa zaidi duniani, huku mshambuliaji mkongwe Cristiano Ronaldo akiendelea kutawala kwa kishindo na kumuacha mbali mpinzani wake wa muda mrefu, Lionel Messi.
Nyota huyo wa klabu ya Al-Nassr ya Saudi Arabia anakadiriwa kuingiza kiasi cha Pauni 225 milioni (takribani Sh1.2 trilioni) kwa mwaka, kupitia mshahara wake mnono klabuni hapo na mikataba minono ya kibiashara. Ronaldo anapata takribani Pauni 187 milioni kutoka Al-Nassr pekee, huku matangazo na biashara vikimuingizia Pauni 37 milioni zaidi — sawa na wastani wa Pauni 488,000 kwa siku!
Messi Shikilia Hapa, Vinara Wengine Waingia Top 5
Nafasi ya pili inashikiliwa na Lionel Messi wa Inter Miami (MLS), anayekusanya takribani Pauni 108 milioni kwa mwaka (Pauni 52 milioni mshahara na Pauni 56 milioni kutoka mikataba ya kibiashara).
Nafasi tano za kwanza zinakamilishwa na mastaa hawa:
-
Kylian Mbappe (Real Madrid) – Pauni 75 milioni kwa mwaka.
-
Erling Haaland (Manchester City) – Pauni 64 milioni kwa mwaka.
-
Vinicius Junior (Real Madrid) – Pauni 56 milioni kwa mwaka.
Vichwa Vipya Kwenye Orodha
Orodha hii ya mwaka 2026 pia imewaleta kwa mara ya kwanza mastaa kama nahodha wa England na Bayern Munich, Harry Kane (nafasi ya tisa kwa Pauni 32 milioni), pamoja na kiungo fundi wa Real Madrid, Jude Bellingham (nafasi ya nane kwa Pauni 34 milioni). Kuongezeka kwa wachezaji hawa kunafanya Uingereza kuwa na wachezaji wawili kwenye orodha hiyo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2013.
Hata hivyo, jina kubwa lililoachwa nje kwenye orodha hii ni mshambuliaji wa zamani wa Real Madrid, Karim Benzema, ambaye kwa sasa hana klabu baada ya kuachana na Al-Hilal.