Maandalizi ya Simba SC
Simba SC

Yote Kuhusu Maandalizi ya Simba SC Rwanda na Afrika Kusini

Vardo October 21, 2026 2:12 pm

Meneja wa Simba SC, Patrick Rweyemamu, ameweka wazi malengo ya kimkakati yaliyofichka nyuma ya kambi zao za maandalizi nchini Rwanda na Afrika Kusini, akisistiza kuwa safari hizo hazikuwa za utalii kama baadhi ya watu walivyodhani, bali zilikuwa na ajenda maalum ya kuimarisha kikosi kiufundi na kiuchezaji.

Akizungumza kabla ya mchezo wao wa leo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya 15 de Agosto ya Equatorial Guinea, Rweyemamu amesema kuwa timu inaendelea kukua na kuimarika kila siku kutokana na kazi kubwa inayofanywa na benchi la ufundi pamoja na morali ya juu ya wachezaji.

Ameeleza kuwa maandalizi hayo yalilenga kuijenga timu ili iwezeimara kukabiliana na ushindani mkali wa msimu huu, ukiwemo mchezo mkubwa wa Kariakoo Derby dhidi ya Yanga na mashindano mbalimbali ya kimataifa.

“Tangu tumeanza ligi, tumecheza takribani mechi saba na mechi mbili za kimataifa. Hii inaweza kuwa mechi yetu ya tatu. Tunaendelea kukua na kuboreka,” amesema Rweyemamu.

Aidha, aliongeza kuwa baadhi ya watu huenda walishindwa kuelewa malengo ya uongozi kufanya maandalizi katika maeneo tofauti, lakini akasisitiza kuwa kila hatua ilipangwa kwa makusudi maalumu ya kiufundi ili kukidhi mahitaji ya ushindani wa msimu huu.

Akizungumzia mchezo wa leo dhidi ya 15 de Agosto, meneja huyo alionyesha imani kubwa kuwa kikosi hicho kitafanya vizuri kutokana na mbinu za makocha na hali ya kujiamini waliyonayo wachezaji.

“Mojawapo ya mechi za mashindano tulizokuwa tunazitegemea ni hii ya leo. Mungu akipenda tukiamka salama, ninaamini tutakuwa bora. Tuko bora kwa sababu ya morali ya wachezaji, ufundi, mbinu na malengo ya walimu. Nadhani tunaonekana vizuri, hivyo tutarajie kufanya vizuri,” alihitimisha Rweyemamu.

Rushine De Reuck Afunguka: Nia Yake ya Kurejea Timu ya Taifa ya Afrika Kusini Inter Milan Kuikaribisha Shakhtar Donetsk, UCL