Steve Barker Simba
Simba SC

Steve Barker Awatonya Simba SC Baada ya Ushindi Mnono CAF Champions League

Vardo October 22, 2026 10:12 am

KOCHA Mkuu wa Simba SC, Steve Barker, amewataka wachezaji wake kutobweteka na matokeo ya kuridhisha kufuatia ushindi mnono wa mabao 6-1 dhidi ya 15 de Agosto ya Equatorial Guinea. Kocha huyo amesisitiza kuwa bado safari ni ndefu na wanapaswa kupambana kwa kiwango kilekile kwenye mchezo wa marudiano ili kufikia malengo yao makubwa katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Wekundu wa Msimbazi Simba walipata ushindi huo mtamu jana Jumatano, Oktoba 21, 2026, katika mchezo wa raundi ya pili ya awali uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, matokeo yaliyowapa mguu mzuri kuelekea mchezo wa marudiano ugenini.

Akizungumzia mchezo huo, Barker alieleza kuwa bao la kusawazisha la wapinzani lilichangia kwa kiasi kikubwa kuufanya mchezo kuwa wazi katika kipindi cha pili, jambo lililoipa nafasi Simba kutumia vizuri kasi ya wachezaji wake wa pembeni kupitia mashambulizi ya kushtukiza (counter-attacks).

“Bao hilo la kusawazisha lilifungua mchezo zaidi katika kipindi cha pili. Timu inapokuwa nyuma kwa mabao, hulazimika kushambulia kutafuta mabao, jambo linalofanya mchezo kuwa wazi. Tuna wachezaji wazuri wenye kasi na nguvu, hali iliyotupa nafasi ya kutumia vizuri uwezo wetu,” amesema Barker.

Kocha huyo aliongeza kuwa lengo lao lilikuwa ni kupata ushindi mkubwa ili kupunguza presha kwenye mchezo wa marudiano, huku wakizingatia ratiba ngumu inayowakabili kwenye ligi ya ndani. Licha ya ushindi huo mkubwa, Barker amewataka wachezaji wake kuondoa dhana ya kuamini kuwa kazi imekwisha.

“Haikuwa suala la kuwaambia wachezaji mambo mengi sana. Tulijua tuna nafasi ya kumaliza kazi yetu na kufanya mchezo unaofuata kuwa rahisi. Hata hivyo, hatupaswi kuingia uwanjani tukidhani utakuwa mteremko. Tunahitaji kuendelea kuonyesha ubora wetu na kucheza kwa nidhamu ileile,” alisisitiza kocha huyo.

Steve Barker Ampa Maagizo Mazito Libasse Gueye Simba Manqoba Mngqithi: Hatua ya Makundi Yanga na Siri ya Udhaifu Wetu