Yanga na TRA United
Yanga SC

Yanga Yamweka Wazi TRA United: Lengo Ni Pointi Tatu Arusha!

Vardo October 22, 2026 8:36 pm

Kikosi cha Yanga kimeweka wazi mikakati yake kuelekea mchezo ujao wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya TRA United, utakaopigwa siku ya Ijumaa, Oktoba 24, mwaka huu, katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Akizungumza kuhusu mchezo huo, Msemaji wa Yanga, Ali Kamwe, ameeleza kuwa timu hiyo imefunga rasmi ukurasa wa mashindano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika na sasa nguvu zote zimeelekezwa kwenye ligi ya ndani ili kuhakikisha wanaondoka na pointi tatu muhimu.

“Tumemaliza mechi yetu ya Ligi ya Mabingwa Afrika na tunaenda Arusha kutafuta pointi tatu katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya TRA United,” amesema Kamwe kwa kujiamini.

Aidha, Kamwe amewajibu wale wote waliokuwa wakidai kuwa kikosi hicho kinapitia wakati mgumu na kinajitafuta, akisisitiza kuwa uongozi na benchi la ufundi linafahamu kile kinachoendelea na matokeo chanya yataonekana hivi karibuni wakati wakitangaza ubingwa.

“Kuna watu walisema Yanga inajitafuta. Waache waseme. Viongozi na benchi la ufundi wanajua wanachokifanya, watakuja kustukia tunatangaza ubingwa,” aliongeza.

Pambano hili linatazamwa kama mtihani mgumu lakini wa kipekee kwa Yanga katika azma yao ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu. Kwa upande wa TRA United, kucheza katika uwanja wa nyumbani mbele ya mashabiki wao wa Arusha kutakuwa ni fursa ya kipekee kutumia mazingira hayo kusaka matokeo chanya na kuzuia kasi ya Wananchi.

Yanga Yamweka Wazi TRA United: Lengo Ni Pointi Tatu Arusha! Simba Yafunguka: Steve Barker Akitaja Siri ya Ushindi Mnono Ligi ya Mabingwa Afrika