Simba Yafunguka: Steve Barker Akitaja Siri ya Ushindi Mnono Ligi ya Mabingwa Afrika
KOCHA Mkuu wa Simba, Steve Barker, amesema ameridhishwa na kiwango kilichoonyeshwa na kikosi chake, akipongeza mchango mkubwa wa wachezaji walioanza mchezo pamoja na wale walioingia kipindi cha pili kuongeza nguvu katika ushindi walioupata dhidi ya 15 de Agosto kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.
Barker ameeleza kuwa Simba ilicheza kwa ustadi na kufunga mabao ya kuvutia, akisisitiza kuwa msingi wa ushindi huo uliwekwa na kikosi cha kwanza, huku wachezaji wa akiba wakiongeza makali baada ya kuingia uwanjani na kubadilisha mchezo.
Kocha huyo aliongoza kwa kusema amefurahishwa zaidi na namna wachezaji waliotoka benchi walivyosaidia timu kufunga mabao mawili, huku kiungo Maurice akitoa mchango mkubwa kwa kutoa pasi ya mwisho (asisti).
“Nina furaha sana. Tumefunga mabao mazuri sana na kwa kweli nadhani msingi uliwekwa na kikosi chetu kilichoanza mchezo. Ilikuwa vizuri pia kuona wachezaji tulioingiza baadaye wakija kusaidia timu na kufunga mabao mawili, huku Maurice akitoa asisti. Hilo ni jambo zuri sana kwetu,” alisema Barker.
Aidha, Barker amesema ushindi huo ni ishara nzuri kwa timu, lakini amewakumbusha wachezaji wake kutoridhika na mafanikio hayo, bali waendelee kujituma kwa bidii ili kujiimarisha zaidi katika michezo ijayo.
Akizungumzia mchezo ujao utakaochezwa Jumapili, kocha huyo alisisitiza kuwa akili na nguvu zao zote zimehamia huko wakilenga kuendeleza wimbi la ushindi na kudumisha kiwango bora walichokionyesha.