Simba SC vs 15 de Agosto
Simba SC

Ahmed Ally Atolea Uvivu Mashabiki wa Simba: “Tukajaze Uwanja wa Uhuru Oktoba 25!”

Vardo October 23, 2026 10:28 am

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, ametoa rai nzito kwa mashabiki na wanachama wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi katika Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam, Jumapili hii ya Oktoba 25, 2026.

Lengo kuu ni kwenda kushuhudia mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya 15 de Agosto, huku akisisitiza kuwa ushindi mnono wa mabao 6-1 uliopatikana ugenini haupaswi kupunguza hamasa ya kuishangilia timu hiyo.

Akizungumza kuhusu mchezo huo, Ahmed alifafanua kuwa pamoja na Wekundu hao wa Msimbazi kuwa na asilimia kubwa ya kutinga hatua ya makundi, kutokwenda uwanjani ni kama kuwanyima wachezaji tuzo ya heshima kwa kazi kubwa waliyoifanya msimu huu.

“Ukiangalia mechi hii, ni kama imeshapoteza mvuto kwa sababu tuna nafasi kubwa ya kwenda makundi, lakini Mwanasimba anatakiwa kuachana na fikra hizo. Tusipoenda uwanjani, maana yake tunawasurubu wachezaji wetu,” alisema Ahmed.

Aidha, meneja huyo aliongeza kuwa Simba ina dhamira ya kuvunja rekodi ya kufuzu kwa mabao mengi zaidi nchini, akisisitiza kuwa hawatakubali kuona timu nyingine ikikaa mbele yao kwa idadi ya mabao ya ushindi wa jumla.

Kuhusu upatikanaji wa tiketi kwa wale ambao hawana simu janja, Ahmed aliwakumbusha kushirikiana na marafiki au majirani zao ili kuhakikisha hakuna siti inayobaki wazi katika uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 18,000 pekee.

Siri ya Nyota wa Simba SC Nathaniel Chilambo Kuwasha Moto Yashtua!