Everton, Newcastle United Kuwania Robo Fainali Carabao Cup
Klabu ya Everton inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Newcastle United katika mchezo wa hatua ya nne ya Kombe la EFL Cup, maarufu kama Carabao Cup, utakaopigwa Alhamisi, Oktoba 29, 2026, saa 22:45 usiku. Mchezo huo utachezwa katika dimba la Hill Dickinson Stadium, jijini Liverpool, huku timu zote zikisaka ushindi utakaowapeleka hatua ya robo fainali ya mashindano hayo.
Everton wataingia katika mchezo huo wakitaka kutumia faida ya kucheza nyumbani ili kuendeleza safari yao ya kuwania kufuzu hatua inayo fuata. Kikosi cha kocha David Moyes kilifuzu hatua hii baada ya kuichapa Wolverhampton Wanderers bao 1-0, lililofungwa na Charly Alcaraz akiwa ametokea benchi. Hata hivyo, Everton wanahitaji kuboresha kiwango chao baada ya kupata matokeo mabaya katika michezo yao ya hivi karibuni ya ligi.
Kwa upande wa Newcastle United, timu hiyo itakuwa na lengo la kuendeleza matumaini ya kutwaa taji la Carabao Cup kwa kupata ushindi ugenini. Newcastle ilitinga hatua hii baada ya kuifunga Millwall bao 1-0 katika raundi iliyopita. Kikosi hicho kitahitaji kutumia uzoefu wake na kuwa makini katika safu ya ushambuliaji ili kuvunja ulinzi wa Everton na kupata nafasi ya kusonga mbele.
Mchezo huu unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na umuhimu wa nafasi ya robo fainali, ambayo inasogeza timu hatua moja karibu na ubingwa. Everton wanaweza kutegemea sapoti ya mashabiki wao,
Huku Newcastle wakitafuta kutumia kasi ya mashambulizi na makosa ya wapinzani. Nidhamu ya safu ya ulinzi, ubunifu wa viungo na umakini katika kutumia nafasi za kufunga vitakuwa miongoni mwa mambo muhimu yatakayoamua matokeo.
Kwa habari na taarifa mbalimbali za michezo usisite kutembelea meridianbet ili upate mambo yote yanayotokea na kuendelea kwenye ulimwengu wakimichezo, ikiwemo michuano mikubwa ya Africa, Ulaya na ile ya falme za kiaarabu zote zinapatikana hapa.
Kwa ujumla, Everton dhidi ya Newcastle United ni pambano ambalo hakuna timu itakayokuwa tayari kukubali kuondolewa kirahisi katika mashindano hayo. Ushindi utaiwezesha timu moja kutinga robo fainali na kuendelea kuota kuhusu kutwaa taji la msimu huu.