Fadlu Davids Yanga SC
Yanga SC

Fadlu Davids Kutua Yanga SC: Kocha wa Zamani wa Simba Kukabidhiwa Mikoba Jangwani

Vardo November 5, 2026 6:38 pm

Klabu ya Yanga SC imeingia katika hatua mpya ya kumsajili aliyekuwa kocha wa zamani wa waporomaji wao Simba SC, Fadlu Davids, ili achukue mikoba ya kukinoa kikosi hicho kufuatia kukwama kwa mazungumzo na kocha Sead Ramovic.

Taarifa za ndani zinathibitisha kuwa Yanga SC na kocha huyo raia wa Afrika Kusini wamefikia makubaliano mazuri ya awali, na kilichobaki sasa ni yeye kuwasili nchini mara baada ya taratibu za mwisho za mkataba kukamilika.

Sababu ya Ramovic Kukosa Dili la Yanga Awali, Yanga ilikuwa mbioni kumtangaza Sead Ramovic kuwa kocha mkuu baada ya kufikia muafaka kamili, ambapo hata tiketi ya ndege kwa ajili ya safari yake ya kuja Tanzania ilishakatwa.

Hata hivyo, Ramovic alipata dharura ya matatizo ya kifamilia yaliyolazimu uwepo wake nyumbani, hali iliyomfanya ashindwe kusafiri kwa wakati uliopangwa. Kutokana na changamoto hiyo, uongozi wa Yanga uliamua kusitisha mazungumzo na kuelekeza nguvu zote kwa Fadlu Davids.

Benchi Jipya la Ufundi Fadlu Davids anatarajiwa kuwasili nchini akiwa ameambatana na benchi lake kamili la ufundi, akiwemo kocha wa viungo na wasaidizi wengine, ili kuanza maandalizi ya kukiimarisha kikosi hicho katika mechi zilizobaki za ligi na mashindano ya kimataifa.

Kuingia kwa Fadlu Davids ndani ya Yanga kinatazamiwa kuleta ushindani mpya na hamasa kubwa kwa mashabiki wa Soka la Bongo kufuatia historia yake katika soka la Kitanzania.

Wakati Mastaa Simba Wakikata Moto Mapema.., Barker Aja na Mpango Huu.., Ligi Kuu Tanzania Bara: Ratiba, Msimamo, Mfumo na Njia za Kimataifa